Pata taarifa kuu
SUDANI-SIASA-USALAMA

Jeshi na upinzani wakubaliana juu ya kuundwa kwa serikali ya mpito

Viongozi wa jeshi na muungano wa upinzani nchini Sudan wamekubaliana juu ya kuundwa kwa serikali ya mpito ambayo itatoa njia kwa kurejeshwa utawala wa kiraia, baada ya rais Omar Hassan Al-Bashir kutimuliwa mamlakani.

Mmoja wa waandamanaji akishikilia bendera ya Sudan. Khartoum, Juni 5, 2019.
Mmoja wa waandamanaji akishikilia bendera ya Sudan. Khartoum, Juni 5, 2019. REUTERS/Stringer
Matangazo ya kibiashara

Umoja wa Afrika (AU) umesema.pande hizo zimeahidi kuunda serikali huru itakayoongozwa kitaalamu pamoja na kuchunguza machafuko ya hvi karibuni yaliyosababisha watu wengi kuuawa.

"Pande mbili zimekubaliana kuunda baraza huru litakalokuwa na rais wa kupokezana baina ya jeshi na raia kwa kipindi cha miaka mitatu au zaidi," msuluhishi wa Umoja wa Afrika, Mohamed Hassan Lebatt, amewaambia wanahabari Ijumaa asubuhi.

Baada ya taarifa hiyo mamia ya watu walimiminika mitaani kwa kushangilia hatua hiyo.

Mazungumzo kati ya pande hizo mbili yaliyoanza mapem awiki hii yalifanyika jijini Khartoum kupitia usuluhishi ulioongozwa na Waziri Mkuu wa Ethiopia na wajumbe wa Umoja wa Afrika.

Mapema Jumatano mchana, katika mkutano na waandishi wa habari, upinzani ulisema uko tayari kushiriki mazungumzo hayo kwa sharti kuwa makubaliano yafikiwe ndani ya saa 72.

Kusitishwa kwa mazungumzo kulisababishwa kwa kiasi kikubwa na muundo wa Baraza la uongozi wa nchi, ambapo kila upande unataka kuongoza.

Kwa mujibu wa vyanzo vilivyo karibu ya mazungumzo hayo, baraza hilo litaundwa na askari 7, raia 7 na mtu mmoja ambaye atachaguliwa na pande hizo mbili. Kwa mujibu wa hati inayojadiliwa, jeshi litaongoza baraza hilo la uongozi wa nchi kwa kipindi cha miezi 18, kabla ya kukabidhi madaraka kwa raia. Kwa Jumla uongozi wa mpito utadumu miaka mitatu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.