Pata taarifa kuu
DRC-SIASA-USALAMA

Mvutano wajitokeza katika muungano wa wa FCC

Nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo kumezuka mgawanyiko ndani ya Muungano wa FCC unaoungwa mkono na rais mstaafu wa nchi hiyo, Joseph Kabila, punde baada ya uteuzi wa Seneta Alexis Thambwe Mwamba, kuwa mgombea wa nafasi ya Rais wa Baraza la Seneti nchini humo.

Seneta Joseph Kabila, aliye kuwa rais wa DRC.
Seneta Joseph Kabila, aliye kuwa rais wa DRC. ©John WESSELS/AFP
Matangazo ya kibiashara

Awali muungano huo ulimpendekeza rais mstaafu Joseph Kabila, lakini baada ya mkutano mkuu wa viongozi wanachama wa muungano wa FCC ikaamliwa kuwa ateuliwe mtu mwengine.

Chama cha AFDC, moja kati ya vyama vinavyounda muungano huo, kimesema kiongozi wake Bahati Lukwebo ndiye mtu anayefaa kwa nafasi hiyo, hatua ambayo  naonyesha huenda kukashuhudiwa mvutano mkubwa wa kisiasa ndani ya FCC.

Seneta Alexis Thambwe Mwamba.
Seneta Alexis Thambwe Mwamba. AFP PHOTO BERTRAND GUAY

Hayo yanajiri wakati muungano mwengine wa upinzani wa Lamuka unakabiliwa na mgawanyiko mkubwa, baada ya kujitokeza mvutano kati ya wafuasi wa Moise Katumbi Chapwe na Martin Fayulu.

Wafuasi wa gavana wa zamani wa Katanga Moïse Katumbi Chapwe wamelaani hatua ya Martin Fayulu ya kuchapisha taarifa bila makubaliano na kiongozi wao.

Hali hiyo inajiri wakati Martin Fayulu na Moise Katimbi Chapwe walisaini taarifa inayotoa wito wa maandamano Juni 30. Wamekuwa hawaelewani kwa miezi kadhaa kuhusu mkakati wa kutumia dhidi ya rais Felix Tshisekedi.

Mmoja wa washirika wa Martin Fayulu ametaja hali hiyo kama jaribio la "kupotosha" wafuasi wake kutoka katika vita yao na hali inayojiri kwa sasa, ambayo ni "kukupinga uhalifu wa polisi dhidi ya maandamano ya raia yaliyofanyika Jumatatu wiki hii."

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.