Pata taarifa kuu
DRC-SIASA-USALAMA

DRC yakumbwa na machafuko wakati ikiadhimisha miaka 59 ya uhuru wake

Polisi jijini Kinshasa nchini DRC, wametumia mabomu ya kutoa machozi siku ya Jumapili, kuwasambaratisha wafuasi wa upinzani waliokuwa wanaandamana wakiongozwa na aliyekuwa mgombea urais Martin Fayulu, huku mtu mmoja akiuawa kwa kupigwa risasi na polisi mjini Goma.

Maafisa wa polisi wakiwapiga wafuasi wa mwanasiasa wa upinzani Martin Fayulu, mgombea wa zamani katika uchaguzi wa urais kupitia muungano wa upinzani wa Lamuka, wakati wa maandamano ya Juni 30, 2019 Kinshasa.
Maafisa wa polisi wakiwapiga wafuasi wa mwanasiasa wa upinzani Martin Fayulu, mgombea wa zamani katika uchaguzi wa urais kupitia muungano wa upinzani wa Lamuka, wakati wa maandamano ya Juni 30, 2019 Kinshasa. © Alexis HUGUET / AFP
Matangazo ya kibiashara

Hali hiyo imetokea wakati nchi hiyo kubwa katika kanda ya Afrika ya Kati ili pokuwa ikiadhimisha miaka 59 ya uhuru wake kutoka mikononi mwa wakoloni Ubelgiji.

Polisi jijini Kinshasa nchini DRC, wametumia mabomu ya kutoa machozi, kuwasambaratisha wafuasi wa upinzani waliokuwa wanaandamana wakiongozwa na aliyekuwa mgombea urais Martin Fayulu, huku mtu mmoja akiuawa kwa kupigwa risasi na polisi mjini Goma.

Gari la Fayulu lilizuiwa na maafisa wa polisi, sawa na mwanasiasa mwingine wa upinzani, Waziri Mkuu wa zamani Adolphe Muzito.

Ripoti zinasema kuwa, polisi zaidi ya 50, walimzingira, Fayulu katika barabara kuu ya Boulevard Lumumba na wakaamua kushuka kuzungumza na mkuu wa jeshi la polisi katika jiji hilo, Sylvano Kasongo.

Maandamano hayo yaliitishwa na Fayulu na Jean Piere Bemba ambaye pia aliwasili nchini humo hivi karibuni akitokea nchini Ubelgiji, kwa kile walichosema ni kuendelea kupinga ushindi wa rais Felix Tshisekedi wakati wa Uchaguzi Mkuu uliofanyika mwezi Desemba mwaka 2018.

Akihojiwa na Televisheni ya France 24, rais Felix Tshisekedi alisema anaunga mkono hatua ya polisi kuzuiwa maandamano hayo, kwa hofu ya machafuko, huku akieleza kuwa  kuna watu ambao hawaelewi maana ya demokrasia na uongozi usiotii sheria.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.