Pata taarifa kuu
SUDANI-SIASA-USALAMA-MAANDAMANO

Viongozi wa maandamano washtumu jeshi kuchelewa kukabidhi madaraka kwa raia Sudani

Viongozi wa maandamano nchini Sudani wameshtumu viongozi wa ngazi ya juu katika jeshi kuchelewesha mchakato wa kukabidhi madaraka kwa raia, na kutishia kuzindua maandamano ya kitaifa na kususia shughuli za serikali.

Waandamanaji waendelea kupiga kambi mbele ya mako makuu ya jeshi Khartoum, Mei 7, 2019.
Waandamanaji waendelea kupiga kambi mbele ya mako makuu ya jeshi Khartoum, Mei 7, 2019. © AFP
Matangazo ya kibiashara

"Mambo tayari yako wazi: kuendelea kupiga kambi mbele ya makao makuu ya jeshi na kuandaa mfumo mwengine wa maandamano ya kususia shughuli za serikali," amesema mmoja wa viongozi hao, Khaled Omar Youssef, kwa waandishi wa habari.

Amesema majibu ya majenerali kuhusu mapendekezo ya kundi lake "yanavunja moyo" na amebaini kwamba majibu hayo yanaweza kuitumbukiza nchi katika hali ya "hatari".

Baraza la Jeshi la Mpito lilichukuwa madaraka Aprili 11 mwaka huu baada ya kumkamata na kumtaka ajiuzulu rais Omar al-Bashir, ambaye alikuwa akikabiliwa na maandamano ya kiraia.

Viongozi wa waandamano wanaendelea kuomba jeshi kukabidhi madaraka kwa raia.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.