Pata taarifa kuu
SUDANI-SIASA-HAKI

Aliyekuwa rais wa Sudani akabiliwa na mashitaka kufadhili makundi ya kigaidi

Mwendesha mashtaka wa Serikali ya Sudani ameagiza kuhojiwa kwa rais wa zamani Omar al-Bashir kuhusiana na tuhuma za utakatishaji wa fedha na kufadhili makundi ya kigaidi, televisheni ya taifa nchini humo imeripoti.

Aliye kuwa rais wa Sudan Omar al-Bashir (Picha ya zamani).
Aliye kuwa rais wa Sudan Omar al-Bashir (Picha ya zamani). REUTERS/Mohamed Nureldin Abdallah
Matangazo ya kibiashara

Bashir ambaye aliingia madarakani kwa mapinduzi ya kiislamu mwaka 1989, ametawala nchi hiyo kwa mkono wa chuma kwa karibu miongo mitatu.

Katika hatua nyingine, mazungumzo kati ya baraza la kijeshi na viongozi wa waandamanaji yamegonga ukuta kwa mara nyingine hali inayotishia kushuhudiwa mzozo zaidi kwenye taifa hilo.

Waandamanaji wanaendelea kuomba jeshi kuachia ngazi na kukabidhi madaraka kwa raia.

Siku chache baada ya muda wa siku 30 kupita bila ya jeshi la Sudan kukabidhi madaraka kwa utawala wa kiraia, umoja wa Afrika umeongeza siku 60 kwa jeshi hilo kufanya hivyo au likabiliwe na vikwazo.

Umoja wa Afrika umetishia kusitisha uanachama wa nchi hiyo ikiwa wanajeshi hawatakabidhi madaraka kwa raia, AU imetoa imelitaka jeshi kuondoka madarakani kuanzia April 15.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.