Pata taarifa kuu
DRC-UN-UCHUNGUZI-HAKI

DRC: Watuhumiwa wawili wa mauaji ya wataalam wa Umoja wa Mataifa watoroka

Watuhumiwa wawili wa mauaji ya wataalam wa wawili Umoja wa Mataifa wametoroka jela katika mji wa Kananga ambako walikuwa wanazuiliwa.

Kulia, Jean Bosco Mukanda, shahidi mkuu, akitoa ushuhuda wake mbele ya Evariste Ilunga, mtuhumiwa mkuu wa kesi ya Kananga.
Kulia, Jean Bosco Mukanda, shahidi mkuu, akitoa ushuhuda wake mbele ya Evariste Ilunga, mtuhumiwa mkuu wa kesi ya Kananga. © Capture d'écran
Matangazo ya kibiashara

Evariste Ilunga, mtu pekee aliyejulikana kwenye mkanda wa video ya mauaji ya wataalam wa umoja wa Mataifa nchini DRC, Michael Sharp (raia wa Marekani) na Zaida Catalan (raia wa Sweden) ni miongoni mwa watuhumiwa hao waliotoroka jela.

Wafungwa watano ndio inaaminiwa kuwa wametoroka jela, kwa mujibu wa mkaguzi mkuu wa jeshi, kwa jumla ya wafungwa 800 wanaozuiliwa katika jela hilo la mji wa Kananga.

Jenerali Munkuntu, kiongozi mkuu wa mashitaka katika ofisi ya Mashitaka ya kijeshi, amesema amepata uthibitisho wa kutoroka kwa wafungwa hao watano. Kati yao, watuhumiwa watatu katika kesi ya mauaji ya wataalam wa Umoja wa Mataifa, ikiwa ni pamoja na wawili ambao wanashtumiwa kuwa walihusika moja kwa moja katika mauaji ya wataalam wawili wa Umoja wa Mataifa. Watu hao ni Evariste Ilunga, anayefahamika kwa jina "beau gars", na mtu anayefahamika kwa jina la "Tshiani". Wawli hao walitoroka na wafungwa ambao walikuwa wamepewa hukumu kubwa.

Ni taarifa mbaya kwa kesi ya Kananga, ambayo imekuwa ikisitishwa na kuahirishwa katika wiki za hivi karibuni kwa sababu mbalimbali. Evariste Ilunga alikuwa anachukuliwa na mahakama ya kijeshi, Umoja wa Mataifa - kama mtuhumiwa mkuu, lakini pia kama shahidi mkuu, kwani ni yeye pekee aliyetambuliwa na polisi ya Umoja wa Mataifa katika mkanda wa video.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.