Pata taarifa kuu
DRC-AJALI-USALAMA

Wakaazi wa Kalehe waomba serikali kuhakikisha usalama wa usafiri wa majini

Rais wa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo Felix Tshisekedi Tshilombo amezuru eneo la ajali ya boti iliyotokea Aprili 15 katika Ziwa Kivu wakati wa safari ya Goma kuelekea Kalehe, mkoani Kivu Kusini. Watu 25 wanadaiwa kupoteza maisha huku watu wengine zaidi ya 150 hawajulikani walipo.

Ajali ya hivi karibu iliyouwa wengi mashariki mwa DRC ilitokea katika Ziwa Kivu (kwenye picha), katika eneo la Kalehe.
Ajali ya hivi karibu iliyouwa wengi mashariki mwa DRC ilitokea katika Ziwa Kivu (kwenye picha), katika eneo la Kalehe. Stéphanie Aglietti/RFI
Matangazo ya kibiashara

Juhudi za kuwatafuta manusura kutokana na ajali ya boti iliozama katika Ziwa Kivu zinaendelea. Duru rasmi za kiusalama zimethibitisha kuwa watu 25 wamepoteza maisha, huku matumaini ya kuwapata watu wakiwa hai yakitoweka.

Katika wilaya ya Kelehe ambako kumetokea ajali hiyo hakuna timu maalum ya uokozi, na wavuvi tu wa eneo hilo ndio waliojitokeza na kutoa msaada wa kuwaokoa watu na kukusanya miili ya watu waliopoteza maisha.

Kaimu Mkuu wa Wilaya hiyo, Oli Bizimungu alielekea katika eneo la tukio na kuorodhesha watu kijiji kwa kijiji na kukosekana watu 96.

Kawaida aina ya mitumbwi hiyo hubeba watu wasiozidi 50 pamoja na mizigo.

Hata hivyo kwa mujibu wa viongozi wa bandari ya Goma watu wasiozidi 40 ndio waliorodheshwa kusafiri na boti hiyo, lakini huenda njiani walichukuwa watu wengine ambapo mashahidi wanasema boti hiyo ilikuwa imepakia kupita kiasi.

Viongozi wa kijeshi wamekwenda kukutana na manusura, ambapo ajali za aina hiyo zimekuwa zikiripotiwa lakini sio kwa idadi kubwa ya watu kiasi hicho. Rais Felix Tshisekedi ameahidi kuanzisha uchunguzi na wahusika wataadhibiwa kwa mujibu wa sheria.

Wanaharakati katika eneo eneo la ajali wamepaza sauti kuitaka serikali kutekeleza jukumu lake kwa kuhakikisha usalama wa usafiri wa majini ambapo kwa asilimia kubwa ajali zinapotokea sababu kubwa inakuwa ni kupakia watu na mizigo kupita kiasi.

Delphin Mbirimbi, mmoja wa wanaharakati wa mashirika ya kiraia katika wilaya ya Kalehe ambae alikutana na manusura wa ajali hiyo anasema wamethibitisha kuwa meli hiyo ilikuwa imebeba watu na mizigo mingi.

Mbali na wanaharakati, wanasiasa pia wamebaini maskitiko yao kutokana na ajali hiyo ambapo asilimia kubwa ya waliopoteza maisha ni kutoka katika eneo la kibiashara la Mukwija, ambako rais Thisekedi na washirika wake wanasubiriwa kuzuri kutathmini chanzo cha ajali za aina hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.