Pata taarifa kuu
IVORY COAST-OUATTARA-GBAGBO-SIASA-ICC

Ouattara: Lazima mtu awajibishwe kwa machafuko ya kisiasa mwaka 2010

Rais wa Ivory Coast Alassane Ouattara amesema haki ni  lazima itendekee kwa waathiriwa wa machafuko ya baada ya Uchaguzi Mkuu mwaka 2010, wakati wa mzozo wa kisiasa kati yake na rais wa zamani Laurent Gbagbo.

Rais wa Ivory Coast  Alassane Ouattara
Rais wa Ivory Coast Alassane Ouattara REUTERS/Afolabi Sotunde
Matangazo ya kibiashara

Ouattara katika mazungumzo maalum na Radio France International jijini Addis Ababa pembezoni mwa mkutano mkuu wa viongozi wa Umoja wa Afrika,  ametoa kauli hii baada ya Mahakama ya Kimataifa ya ICC kumfutia mashtaka rais wa zamani Laurent Gbagbo.

“Lazima mtu awajibike kwa kusababisha mauaji ya watu 3,000, natumai haki itatendeka, hiki ndicho wanachotaka waathiriwa wa machafuko hayo,” alisema rais Ouattara.

Aidha, amekanusha madai kuwa serikali yake ilishirikiana na upande wa mashtaka katika Mahakama hiyo kumzuia Gbagbo kwa muda mrefu kizuizini,  tangu mwaka 2011.

Badala yake, ameongeza kuwa, serikali yake inaendelea na uchunguzi kubaini waliohusika kuchochea na kufadhili  machafuko hayo na kusababisha maafa.

Mwezi Januari, Mahakama ya ICC limwachilia huru Gbagbo na msaidizi wake Charles Ble Goude baada ya kuwafutia mashtaka ya kuchochea mauaji hayo ya kisiasa.

Licha ya kuachiliwa huru, Gbagbo amezuiwa na Mahakama ya ICC kurejea nyumbani na amekabidhiwa kwa serikali ya Ubelgiji.

Kuelekea Uchaguzi Mkuu mwaka 2020, rais Ouattara hajaweka wazi iwapo atawania tena.

“Iko wazi kuwa naweza kuwania iwapo nataka. Tuna katiba mwaka 2016 na naweza nikiamua, “ amesema raia Ouattara.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.