ERITREA-ETHIOPIA-USHIRIKIANO
Rais wa Eritrea apongeza juhudi za Waziri Mkuu wa Ethiopia
Rais wa Eritrea Isaias Afwerki anasema nchi yake na Ethiopia, zimejengeana kuaminiana baada ya kutia saini mkataba mpya wa ushirikiano mwezi Julai.
Imechapishwa:
Matangazo ya kibiashara
Hata hivyo, rais Afwerki amesema mataifa hayo mawili bado yanahitaji kusuluhisha baadhi ya mambo ili kuimarisha zaidi uhusiano huo mpya.
Eritrea na Ethiopia zilitiliana saini makumbaliano katika mkutano nchini Saudi Arabia ya kuboresha uhusiano baina ya nchi hizo mbili zilizowahi kuwa kwenye mvutano kwa miaka 20.
Tangu mwaka 1998, matafa hayo yalianza kutofautiana kuhusu biashara na baadaye kulifuatia vita vya kuwania mpaka, vilivyosababisha vifo vya watu 80,000.