Pata taarifa kuu
ERITREA-ETHIOPIA-USHIRIKIANO

Eritrea yafungua ubalozi wake Ethiopia

Rais wa Eritrea Issaias Afeworki amefungua Jumatatu wiki hii ubalozi wa nchi yake nchini Ethiopia, ubalozi ambao uliendelea kufungwa kwa miaka 20 baada ya kuzuka uhasama wa uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi hizi mbili jirani za Pembe la Afrika.

Rais wa Eritrea, Issaias Afeworki.
Rais wa Eritrea, Issaias Afeworki. Reuters
Matangazo ya kibiashara

Ufunguzi wa ubalozi huu Addis Ababa unahitmisha siku tatu za ziara rasmi ya rais wa Eritrea nchini Ethiopia. Ufunguzi ambao unalenga kukuza uhusiano na kusitisha vita vya miaka ishirini kati ya nchi hizo mbili.

Ziara hiyo ilikuja siku chache baada ya kusainiwa Julai 9 huko Asmara, wakati wa ziara ya Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed, "tamko la pamoja la amani na ushirikiano" ambalo lilimaliza miaka miwili nchi hizi mbili zikiwa katika mgogoro mkubwa wa kivita.

Picha zilizorushwa na televisheni ya Ethiopia EBC zimeonyesha Bw Isaias akipandisha bendera ya Eritrea na kukubali kupokea funguzo za jengo la ubalozi kutoka mikononi mwa Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed.

Katika siku hizi tatu za ziara yake, Bw Issaias pia alitembelea Hifadhi muhimu ya viwanda na kuchangia chakula cha jioni na tamasha iliyohudhuria na maelfu ya wananchi wa Ethiopia.

EBC inaarifu kuwa rais wa Eritrea aliondoka Addis Ababa na kurudi Asmara mara baada ya sherehe za ufunguzi wa ubalozi wa Eritrea nchini Ethiopia.

Ethiopia na Eritrea waliwafukuza wanadiplomasia wao mwanzoni mwa vita kati ya mwaka 1998 na 2000, hasa kwa sababu ya kutokubaliana kuhusu mpaka wao wa pamoja, vita ambavyo vilisababisha vifo vya watu 80,000.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.