Pata taarifa kuu
DRC-Mwosengo-KANISA

Kardinali Laurent Monsengwo astaafu

Mkuu wa Kanisa Katoliki nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Kardinali Laurent Pasinya Monsengwo, mmoja wa wakosoaji wakuu wa upinzani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, amestaafu.

Laurent Pasinya Monsengwomuda mfupi baada ya kuteuliwa kwenye nafasi ya kardinali Novemba 2010.
Laurent Pasinya Monsengwomuda mfupi baada ya kuteuliwa kwenye nafasi ya kardinali Novemba 2010. VINCENZO PINTO / AFP
Matangazo ya kibiashara

Ripoti zinasema kuwa, kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis amekubali uamuzi wa Kadinali Mosengwo, kujiuzulu akiwa na umri wa miaka 79.

Mosengwo amekuwa katika mstari wa mbele kushinikiza mabadiliko ya kisiasa nchini DRC, na kumshinikiza rais Joseph Kabila kutowania urais kwa muhula wa tatu.

Ameachia nafasi hiyo wakati DRC ikisubiri Uchaguzi Mkuu tarehe 23 mwezi ujao.

Kardinali Laurent Monsengwo mwenye umri wa miaka 79 alikuwa mmoja wa wakosoaji dhidi tawala mbalimbali za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (Zaire ya zamani), tangu utawala wa dikteta Mobutu Sese Seko (1965-1997), utawala wa Laurent-Désiré Kabila (1997-2001), hadi utawala wa Joseph Kabila.

"Watu wasiofaa wanapaswa kuachia nafasi haraka," alisema baada ya vikosi vya usalama kuzimakwa ukatili moja ya maandamano ya kwanza ya kumshinikiza Rais Joseph Kabila kuachia ngazi, Desemba 31, 2017. Katika ghasia hizo watu sita waliuawa mjini Kinshasa, baada ya uchaguzi kuahirishwa kwa mara ya pili nchini DRC.

Akijibu dhidi ya tuhuma hizo, Rais Joseph Kabila alishutumu Kanisa Katoliki kuingilia masuala ya kisiasa nchini DRC katika mkutano na waandishi wa habari Januari 26.

"Kati ya mwezi Desemba 2017 na Februari 2018, waumini wa Kanisa Katoliki waliandamana mara tatu nchini DRC wakipinga rais Joseph Kabila kusalia madarakani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.