Pata taarifa kuu
DRC-UCHAGUZI-SIASA

Magari ya jeshi kutumika katika uchaguzi wa Desemba DRC

Tume ya Uchaguzi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imepokea malori na ndege za jeshi vitakavyosafirisha vifaa vya uchaguzi wa mwezi Desemba, kulingana na nia njema ya DRC ya kutoa msaada wowote wa kimataifa kwa uchaguzi huo, kwa mujibu wa serikali ya DRC.

Dereva wa jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (FARDC) mbele ya malori ya kijeshi kwenye barabara kuu Oktoba 29, 2018 Kinshasa.
Dereva wa jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (FARDC) mbele ya malori ya kijeshi kwenye barabara kuu Oktoba 29, 2018 Kinshasa. © AFP
Matangazo ya kibiashara

Magari mia moja na hamsini aina ya Kamaz yaliyotengenezwa Urusi yameegeshwa mbele ya makao makuu ya tume huru ya uchaguzi CENI.

Ndege kadhaa na helikopta pia zimekabidhiwa Tume ya Uchaguzi (CENI) wakati wa sherehe rasmi iliyofanyika kenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Ndjili mashariki mwa mji wa Kinshasa.

"Vifaa hivi ni vya jeshi la DRC na baada ya uchaguzi, vitarudishwa kwenye kambi vilikotoka," amesema Crispin Atama Thabe, Waziri wa Ulinzi wa DRC.

" Hii ni kutokana na uhuru wa nchi yetu, ni nia njema ya serikali kuona CENI inafanya shughuli zake ikijitegemea na ikiwa huru, bila kutegemea misaada kutoka nje ya nchi kwa kutekeleza wajibu wake ", Waziri wa Mambo ya Ndani Henri Mova, amesema.

Kwa ishara hii, serikali inataka "jamii ya kimataifa kuheshima DRC kama taiafa huru linalojitegemea", Bw Mova ameongeza.

Serikali ya DRC iliahidi kufadhili uchaguzi wake peke yake bila msaada kutoka nje, licha ya mapendekezo ya msaada kutoka kwa jumuiya ya kimataifa.

Uchaguzi Mkuu utaojumuisha uchaguzi wa urais, uchaguzi wa wabunge na uchaguzi wa magavana utafanyika tarehe 23 Desemba baada ya kuahirishwa mara mbili: mwishoni mwa mwaka 2016 na mwishoni mwa mwaka 2017.

Wagombea ishirini na moja watawania katika uchaguzi huo kumrithi Rais Joseph Kabila, ambaye anasalia na miezi kumi nane ya kuongoza nchi hiyo kubwa Afrika ya Kati, yenye ukubwa wa kilomita mraba milioni 2.3.

Kabila alimteua waziri wake wa zamani wa mambo ya ndani, Emmanuel Ramazani Shadary, kama mgombea wa wengi katika uchaguzi wa rais. Wapinzani wanataka kuwasilisha mgombea mmoja lakini bado hawajaweza kukubaliana kuhusu jina la mgombea huyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.