Pata taarifa kuu
DRC-BURUNDI-USALAMA

Usalama waanza kurejea kwenye eneo la mpakani kati ya Burundi na DRC

Usalama umerejea kwenye bonde la Ruzizi baada ya kuripotiwa mapigano kati ya jeshi la Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo FARDC na wapiganaji waasi wa kundi la FNL kutoka nchini Burundi ambao walivuka mpaka.

Askari wa Burundi wakipiga doria karibu na msitu wa Rukoko, karibu na mpaka na DRC.
Askari wa Burundi wakipiga doria karibu na msitu wa Rukoko, karibu na mpaka na DRC. AFP / Esdras Ndikumana
Matangazo ya kibiashara

Usiku wa Ijumaa kuamkia Jumamosi kundi la watu wenye silaha wanaodhaniwa kuwa wapiganaji wa FNL walivuka mpaka na kushambulia zahanai moja katika kijiji cha Nyamitanga, magharibi mwa Burundi, kilomita 50 kutoka mji mkii Bujumhura.

Askai zaidi ya sita waliuawa katika mapigano hayo ambayo, hayakudaiwa na kundi hata moja, kwa mujibu wa mashahidi na baadhi ya vyanzo vya kijeshi vya Burundi.

Hata hivyo jeshi la Burundi lilisem akuwa askari wawili ndio walishambuliwa katika mashambulizi hayo, huku silaha kadhaa za wapiganaji hao zikikamatwa.

Hali ya usalama si ya kuridhisha katika eneo la bonde la Rusisi, mto unatenganisha Burundi na DRC. Makundi ya waasi wa Burundi yamekuwa yakitokea nchini DRC na kufanya mashambulizi nchini Burundi.

Hata hivyo kwa mujibu wa vyanzo kadhaa kutoka DRC, makundi ya waasi wa Burundi yanashirikiana na baadhi ya makundi ya waasi nchini DRC kwa kufanya mashambulizi katika maeneo ya mpakani kati ya nchi hizi mbili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.