Pata taarifa kuu
LIBYA-USALAMA

Askari wanne wauawa katika shambulio Libya

Askari wanne wameuawa na wengine watatu kujeruhiwa Alhamisi wiki hii katika shambulizi dhidi ya kituo cha ukaguzi karibu na mji wa Zliten, amesema meya wa Zliten, magharibi Libya

Shambulizi dhidi ya kituo cha mafunzo chaa polisi katika mji wa Zliten, Libya, Januari 7, 2015.
Shambulizi dhidi ya kituo cha mafunzo chaa polisi katika mji wa Zliten, Libya, Januari 7, 2015. © AFP
Matangazo ya kibiashara

"Shambulizi hilo lililenga kikosi maalum cha Wizara ya Mambo ya Ndani (...) kwenye kituo cha ukaguzi cha Wadi Kaam, na kusasbabisha vifo vya watu wanne na wengine watano kujeruhiwa," AFP Moftah Ahmadi ameliambia shirika la habari la AFP.

Kwa mujibu wa Ahmadi, shambulio hilo lilitokea mapema asubuhi na liliendeshwa na watu watatu "wakitumia silaha ndogo na gruneti". Mmoja wa washambuliaji alipigwa risasi wakati wa ufyatulianaji risasi na vikosi vya usalama, na wengine wawili walitoweka.

kituo cha ukaguzi kilicholengwa kinapatikana kwenye barabara ya pwani kati ya Khoms (kilomita 115 mashariki mwa Tripoli) na Zliten (kilomita 170 mashariki mwa Tripoli), katika eneo ambalo kundi la Islamic State (IS) limeweka mizizi yake.

Lakini hakuna kundi hata moja ambalo limedai kuhusika na shambulizi hili.

Tangu kuanguka kwa utawala wa Muammar Gaddafi mnamo mwaka 2011, Libya inaendelea kukabiliwa na vita kati ya makundi ya watu wenye silaha.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.