Pata taarifa kuu
LIBYA-SIASA-USALAMA

Uchaguzi mkuu kufanyika Desemba 10, 2018 nchini Libya

Viongozi wanne wakuu katika mgogoro wa Libya waliokutana Jumanne wiki hii nchini Ufaransa kwa jitihada za rais wa nchi hiyo Emmanuel Macron, wamefikia mkataba na kukubaliana tarehe ya Uchaguzi mkuu. Uchaguzi mkuu umepangwa kufanyika tarehe 10 Desemba 2018.

Mkutano wa kimataifa kuhusu Libya, wakihudhuria viongozi wa nchi jirani na Libya, wawakilishi wa nchi za Ulaya na Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron, Elysee huko Paris.
Mkutano wa kimataifa kuhusu Libya, wakihudhuria viongozi wa nchi jirani na Libya, wawakilishi wa nchi za Ulaya na Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron, Elysee huko Paris. Reuters
Matangazo ya kibiashara

"Tunaahidi kufanya kazi kwa ufanisi na Umoja wa Mataifa kwa minajili ya kufanya uchaguzi wa kuaminika na wa amani na kuheshimu matokeo ya uchaguzi," imesema taarifa ya pamoja baada ya mkutano katika ikulu ya Elysee.

Viongozi wakuu wanne kutoka Libya waliokutana na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, wameahidi kufanya kazi pamoja ili Uchaguzi mkuu uweze kufanyika mnamo Desemba 10 mwaka huu, kulingana na taarifa iliyosomwa baada ya mkutano huo.

"Tunaahidi (...) kufanya kazi kwa ufanisi na Umoja wa Mataifa kwa minajili ya kufanyika uchaguzi wa kuaminika na wa amani (...) na kuheshimu matokeo ya uchaguzi", inasema "taarifa ya kisiasa" iliyoidhinishwa na Kiongozi wa serikali ya umoja Fayez al-Sarraj, Marshal Khalifa Haftar, anayetawala Mashariki mwa nchi, Spika wa bunge, Aguila Salah, na rais wa Baraza Kuu la Nchi, Khaled al-Mechri.

Libya imeendelea kukosa amani, huku wanajeshi wa serikali wakiendelea kupambana na makundi ya waasi tangu kuuawa kwa kiongozi wa nchi hiyo Muammar Gaddafi mwaka 2011.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.