Pata taarifa kuu
CAMEROON-UN-USALAMA

UN: Watu waendelea kutoroka makaazi yao Cameroon

Umoja wa Mataifa unasema idadi ya raia wa Cameroon wanaokimbia kutoka eneo linalozungumza lugha ya Kiingereza, inaongezeka. Watu zaidi ya Laki Mbili, tayari wameyakimbia makwao Magharibu mwa nchi hiyo kuanzia mwaka uliopita, huku elfu 21 wakienda nchini Nigeria.

Mamlaka ya Cameroon ilizima mtandao wa internet katika mikoa wanakozungumza Kiingereza.
Mamlaka ya Cameroon ilizima mtandao wa internet katika mikoa wanakozungumza Kiingereza. Photo: Michael Bocchieri/Getty Images/AFP
Matangazo ya kibiashara

Wanahakarati kutoka eneo hilo wanataka kujitenga na kuunda nchi yao wanayosema wanataka iitwe Ambazonia, kwa sababu ya kuendelea kutengwa na serikali ya Yaounde.

Hata hivyo, serikali ya Yaounde imeendelea kusisitiza kuwa, Kusini mwa nchi hiyo ni Cameroon na madai ya wanaharakati hayo hayawezi kupewa nafasi.

Maelfu ya raia wa Cameroon wanaozungumza Kiingereza wamekimbilia nchini Nigeria kwa wasiwasi wa kuuwawa kutokana na makabiliano kati ya maafisa wa usalama na wanaharakati.

Hivi karibuni msafara wa magari uliokuwa unamsafirisha Waziri wa Ulinzi wa Cameroon Joseph Beti Assomo umeshambuliwa katika eneo ambalo kuna wazungumzaji wa lugha ya Kiingereza.

 

 

 

 

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.