Pata taarifa kuu
CAMEROON-USALAMA

Msafara wa Waziri wa Ulinzi wa Cameroon washambuliwa

Waziri wa ulinzi wa Cameroon Joseph Beti Assomo amenusurika kifo baada ya kundi la watu wenye silaha kuushambulia msafara wake katika mji wa Kumba, mji wenye watu wengi wanaozungumza Kiingereza, Kusini Magharibi mwa Cameroon.

Wakimbizi wa Cameroon, hapa ni katika kambi ya Bashu-Okpambe, Jimbo la Cross Rivers, kusini magharibi mwa Nigeria, Januari 31, 2018.
Wakimbizi wa Cameroon, hapa ni katika kambi ya Bashu-Okpambe, Jimbo la Cross Rivers, kusini magharibi mwa Nigeria, Januari 31, 2018. © PIUS UTOMI EKPEI / AFP
Matangazo ya kibiashara

Shambulio hilo limefanyika wakati jeshi la nchi hiyo likiendelea na Mapigano tangu siku ya Jumatano usiku na Alhamisi asubuhi wiki hii na wanaharakati wanaotaka eneo hilo kujitenga waliokua wakibebelea silaha.

Taarifa zaidi zinasema watu wengi, ikiwa ni pamoja raia wa kawaida, wameuawa katika mapigano hayo huko Kumba tangu siku ya Jumatatu, chanzo cha hospitali kimeliambia shirika la habari la AFP.

Chanzo hicho kimebaini kuwa "watu hao wameuawa katika operesheni mbalimbali za jeshi" kufuatia kuawa siku ya watu kwa kamanda wa polisi katika mji wa Kumba, mauaji yanayodaiwa kutekelezwa na wanaharakati wanaotaka kujitenga kwa maeneo yao.

Tangu kifo cha afisa huyo wa polisi, hali ya usalama imeendelea kudorora katika mji huo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.