Pata taarifa kuu
ETHIOPIA-ERITREA-USHIRIKIANO

Ndege za Ethiopia Airlines kuanza safari kwenda Asmara Julai 17

Shirika la ndege la Ethiopia, Ethiopia Airlines, limetangaza Jumanne wiki hii kwamba ndege zake zitaanza kufanya safari kuelekea Asmara, mji mkuu wa Eritrea, Julai 17 baada ya nchi hizi mbili kufufua uhusiano wa kidiplomasia.

Ndege za shirika la kitaifa la ndege la Ethiopia, Ethiopia Airlines, zatarajia kuanza safari kuelekea Asmara, mji mkuu wa Eritrea, baada ya nchi hizi mbili kufufua uhusiano wa kidiplomasia.
Ndege za shirika la kitaifa la ndege la Ethiopia, Ethiopia Airlines, zatarajia kuanza safari kuelekea Asmara, mji mkuu wa Eritrea, baada ya nchi hizi mbili kufufua uhusiano wa kidiplomasia. REUTERS/Amr Abdallah Dalsh
Matangazo ya kibiashara

Siku ya Jumatatu Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed na Rais wa Eritrea Isaias Afwerki walitia saini kwenye "tamko la pamoja la amani na urafiki" huko Asmara kuashiria mwisho wa vita vya miaka 20 kati ya nchi hizo mbili.

Serikali za Addis Ababa na Asmara wamekubaliana kufufua uhusiano wa kidiplomasia kwa kufungua balozi zao, kuanzisha upya safari za ndege kati ya nchi hizo mbili na kushirikiana ili kuendeleza bandari ya Eritrea.

"Kwa ufunguzi wa ukurasa mpya wa amani na urafiki kati ya nchi hizi mbili, tunatarajia kurejesha safari za ndege aina ya Boeing 787 kuelekea Asmara," amesema Tewolde GebreMariam, meneja mkuu wa kampuni ya Ethiopia Airlines.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.