Pata taarifa kuu
LIBYA-USALAMA

Watu 11 wauawa katika shambulizi dhidi ya tume ya uchaguzi Tripoli

Watu wasiopungua 11 wameuawa Jumatano wiki hii katika shambulizi linalodaiwa kutekelezwa na washambuliaji wa kujitoa mhanga dhidi ya makao makuu ya tume ya uchaguzi nchini Libya. Shambulizi hilo lilitokea katika mji mkuu wa nchi hiyo, Tripoli, vyanzo vya usalama vimesema.

Eneo la shambulizi la kujitoa mhanga dhidi ya tume ya uchaguzi huko Tripoli, Libya, Mei 2, 2018.
Eneo la shambulizi la kujitoa mhanga dhidi ya tume ya uchaguzi huko Tripoli, Libya, Mei 2, 2018. REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Washambuliaji waliweza kuingia katika majengo ya tume ya uchaguzi, msemaji wa tume hiyo amesema. "Niliona washambuliaji wawili wa kujitoa mhanga wakisema kwa sauti kubwa Allah Akbar (Mwenyezi Mungu ni Mkubwa)," amesema Khaled Omar.

"Mshambuliaji mmoja wa kujitoa mhanga alijilipua ndani ya majengo ya tume ya uchaguzi na wengine walichoma moto sehemu moja ya jengo hilo," ameongeza.

Kulikuepo na ufyatulianaji risasi na vikosi vya usalama. Wafanyakazi waliweza kuondoka jengo hilo. Lakini wafanyakazi watatu waliuawa, pamoja na polisi wanne, Khaled Omar amesema.

Wizara ya Afya imetaoa ripoti ya watu 11 waliouawa na wawili waliojeruhiwa.

Picha zilizorushwa kwenye mitandao ya kijamii zinaonyesha moshi mweusi ukiwa juu ya kata ya Tripoli ambapo tume ya uchaguzi inapatikana.

Shambulizi hili ni la aina yake mjini Tripoli kwa miaka kadhaa sasa. Vurugu katika mji mkuu hivi karibuni zililkua zilipungua na kulikua kukishuhudiwa mapigano kati ya makundi hasimu.

Tume inafanya kazi kwa orodha ya wapigakura kuelekea uchaguzi mpya, ambao Umoja wa Mataifa unatarajia utafanyika mwishoni mwa mwaka huu.

Karibu wapiga kura wapya milioni moja wameorodheshwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.