Pata taarifa kuu
DRC-HWO-EBOLA-AFYA

WHO yaonya kuhusu kuongezeka kwa hatari ya Ebola DRC

Shirika la Afya Duniani (WHO) limetangaza leo Ijumaa asubuhi kuwa limefanya tathmini mpya na kubaini kwamba hatari ya Ebola imeongezeka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).

Vifaa vya kukabiliana na Ebola kabla ya kusafirishwa kwenda DRC.
Vifaa vya kukabiliana na Ebola kabla ya kusafirishwa kwenda DRC. REUTERS/MEDECINS SANS FRONTIERES (MSF)
Matangazo ya kibiashara

Shirika lhili a Afya la Umma la Umoja wa Mataifa sasa linaona kwamba hatari ya afya ya umma inayotokana na Ebola iko "juu sana", dhidi ya "kiwango" hicho katika tathmini yake ya awali. Vile vile, hatari ya kikanda, ikiwa ni pamoja na majirani wa DRC, imetoka kwenye kiwango cha "wastani" hadi kufikia kiwango cha "juu zaidi".

Tathimini hiyo mpya ni matokeo ya uthibitisho wa kesi ya kwanza ya ugonjwa huo katika mji wa Mbandaka, iliyotangazwa siku ya Jumatano jioni na Wizara ya Afya ya DRC.

Ugonjwa wa Ebola umeua watu 23 katika maeneo mbali mbali nchini DRC.

Hii ni mara ya tisa DRC ikikabiliwa na ugonjwa wa Ebola. Ugonjwa huo ulionekana kwa mara ya kwanza karibu na Mto Ebola kaskazini mwa nchi katika miaka ya 1970.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.