Pata taarifa kuu
ETHIOPIA

Chama tawala Ethiopia kimechagua waziri mkuu mpya

Muungano wa vyama vinavyounda Serikali nchini Ethiopia vimemchagua Abiy Ahmed kutoka kwenye kabila kubwa la Oromom uteuzi ambao umetoa fursa ya yeye kuwa waziri mkuu.

Waziri mkuu wa Ethiopia, Hailemariam Desalegn.
Waziri mkuu wa Ethiopia, Hailemariam Desalegn. REUTERS/Tiksa Negeri
Matangazo ya kibiashara

Kama kiongozi wa chama cha Ethiopian Revolutionary Democratic Front, Abiy anatarajiwa kuchukua madaraka kutoka kwa Hailemariam Desalegn ambaye alitangaza kujiuzulu mwezi uliopita katika uamuzi wa kushtukiza baada ya miaka miwili ya maandamano kuipinga Serikali.

"Baraza la EPRDF limemchagua Dr Abiy Ahmed kama kiongozi wa chama," imesema taarifa ya kituo cha televisheni ya taifa.

Abiy atakuwa waziri mkuu wa kwanza kutoka kabila la Oromo katika kipindi cha miaka 27 ya utawala wa chama cha EPRDF ambacho tangu kuingia kwake madarakani kimefanikiwa kubadili uchumi wa taifa hilo.

Licha ya mvutano wa kikabila wananchi wengi wa Ethiopia wana imani kuwa Abiy atabadili uelekeo wa chama tawala ambacho kilichukua madaraka mwaka 1991 kutoka kwa utawala wa kijeshi.

Mwaka 2015 hasira dhidi ya chama tawala iliongezeka na kusababisha wanaharakati wa eneo la Oromo kuanzisha maandamani ya kuipinga Serikali maandamano ambayo yameshuhudia mamia ya watu wakipoteza maisha.

Kabila la pili kwa ukubwa nchini humo la Amharas baadae walijiunga kwenye maandamano ambayo hata hivyo lilijiondoa baada ya Serikali kutangaza miezi 10 ya hali ya hatari.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.