Pata taarifa kuu
HAGUE

Germain Katanga aondoa rufaa yake katika Mahakama ya Kimataifa ya ICC

Aliyekuwa kiongozi wa waasi Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo katika Jimbo la Ituri Germain Katanga aliyehukumiwa jela miaka 12 na Mahakama ya Kimataifa ya ICC ameondoa rufaa dhidi ya hukumu yake.

Germain Katanga
Germain Katanga AFP PHOTO / ANP / POOL
Matangazo ya kibiashara

Majaji katika Mahakama hiyo, walimkuta Katanga na hatia ya kulifadhili kundi la waasi la FRPI waliotekeleza mauaji makubwa na ubakaji wa wanawake mwaka 2003 katika Jimbo hilo.

Mawakili wa Katanga, wameifahamisha Mahakama ya rufaa kuwa Katanga ameamua kuondoa rufaa hiyo na amekubali hukumu iliyotolewa dhidi yake na Mahakama.

Katanga mwenye umri wa miaka 36 alihukumiwa na Mahakama hiyo mwezi wa Machi mwaka huu baada ya kupatikana na kosa la ukiukwaji wa haki za Binadamu dhidi ya wakazi wa kijiji cha Bogoro huku zaidi ya 200 wakipoteza maisha.

Mkaazi wa Jimbo la Ituri
Mkaazi wa Jimbo la Ituri AFP PHOTO / LIONEL HEALING

Majaji walimpa hukumu hiyo, baada ya zaidi ya miaka saba ya kuzuiliwa na kuamua kuwa atakitumkia tu kifungo cha miaka mitano inayosalia.

Hukumu dhidi ya Katanga ilikuwa ya pili kutolewa katika historia ya Mahakama hiyo ya Kimataifa.

Mahakama ya ICC ilitoa hukumu yake ya kwanza mwaka 2012 dhidi ya kiongozi mwingine wa waasi nchini DRC Thomas Lubanga, aliyefungwa jela miaka 14.

Vita katika Jimbo la Ituri yalianza kushuhudiwa tangu mwaka 1999, na kusabisha vifo vya zaidi ya watu 60,000 kwa mujibu wa Mashirika ya kutetea haki za binadamu.

Germain Katanga alikamatwa mwaka 2005 na kufikishwa katika Mahakama ya Kimataifa ya ICC mwaka 2007 kufunguliwa mashtaka.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.