Pata taarifa kuu
CONGO BRAZZAVILLE-USALAMA

Watu kadhaa wakamatwa kwa madai ya kutaka kupindua serikali Congo

Afisa mmoja wa juu wa jeshi la Congo ambaye pia alikuwa mtu wa karibu wa rais Denis Sassou Nguesso amekamatwa jijini Brazzaville akituhumiwa kupanga njama za kutaka kuipindua Serikali.

Jenerali Norbert Dabira, mwaka 2005, wakati wa kesi ya watu "waliotoweka kwenye pwani" huko Brazzaville, wakati ambapo aliachiliwa huru.
Jenerali Norbert Dabira, mwaka 2005, wakati wa kesi ya watu "waliotoweka kwenye pwani" huko Brazzaville, wakati ambapo aliachiliwa huru. AFP PHOTO / GG Kitina
Matangazo ya kibiashara

Taarifa kutoka nchini humo na kuthibitishwa na watu wa karibu kwenye Serikali, zinasema kuwa Jenerali Norbert Dabira alikamatwa Jumatano ya wiki hii na polisi na toka wakati huo amekuwa akihojiwa na kikosi maalumu cha idara ya usalama wa taifa.

Afisa mmoja wa jeshi ambaye hakupenda kutaja jina lake amesema kuwa tuhuma dhidi ya Dabira zinahusu jaribio analodaiwa kuwa alilipanga mwaka 2017 kumpindua rais Sassous Nguesso.

Kukamatwa kwa Jenerali Dabira kunakuja wakati huu ambapo Serikali inawatuhumu wanasiasa wa upinzani kwa kujaribu kuhatarisha usalama wa taifa na kuzusha vurugu ambapo mpaka sasa wanasiasa kadhaa wanashikiliwa.

Watu wengine wanaoshikiliwa sambamba na Jenerali Dabira ni pamoja na aliyekuwa mkuu wa utawala wa jeshi la nchi hiyo Jenerali Jean-Marie Michel Mokoko na waziri wa zamani Andre Okombi Salissa ambao wote waligombea urais mwaka 2016.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.