Wanahabari wa RFI an AFP washambuliwa na polisi Brazzaville
Polisi waliokuwa wamevalia nguo za kiraia waliwavamia wanahabari waliokuwa wanakutana na Wakili wa mwanasiasa wa upinzani Andre Okombi Salissa nchini jijini Brazaville nchini Congo Brazaville.
Imechapishwa:
Ripota wa RFI na AFP Loïcia Martial amethibitisha kuvamiwa kwao, kabla ya mkutano huo kuanza.
Wanahabari hao walipigwa na kupokonywa vifaa vyao vya kazi.
Okombi ambaye alikuwa mpinzani wa rais Denis Sassou Ngueso wakati wa uchaguzi wa urais mwaka uliopita, anazuiliwa kwa madai ya kuhatarisha usalama wa nchi hiyo.
RFI na shirika la habari la AFP wanalaani kitendo hicho kiovu dhidi ya mwanahabari wao.
RFI na shirika la habari la AFP wanaomba wanahabari hao warudishiwe vifaa vyao vya kazi.