Pata taarifa kuu
LIBERIA-UCHAGUZI-SIASA

Matokeo ya uchaguzi wa urais kutolewa Alhamisi hii

Matokeo ya awali ya uchaguzi wa marudio wa urais nchini Liberia yanatarajiwa leo Alhamisi, katika hatua ya kihistoria ya kubadilishana madaraka kidemokrasia kwa mara ya kwanza katika taifa hilo baada ya miaka mingi.

Wananchi wa Liberia wanaendelea kusubiri matokeo ya uchaguzi wa urais uliofanyika Jumanne Desemba 26, 2017.
Wananchi wa Liberia wanaendelea kusubiri matokeo ya uchaguzi wa urais uliofanyika Jumanne Desemba 26, 2017. REUTERS/Thierry Gouegnon
Matangazo ya kibiashara

Ushindani ni kati ya mwanasoka wa zamani George Weah dhidi ya Makamu wa Rais Joseph Boakai.

Yeyote atakayeshinda atamrithi mwanamke wa kwanza kuchaguliwa kuwa rais barani Afrika bi Ellen Johnson Sirleaf, ambaye alichaguliwa kuongoza taifa hilo dogo la Afrika Magharibi mwaka 2006.

Mtangulizi wa Sirleaf, Charles Taylor alikimbia nchi mwaka 2003, akiwa na matumaini ya kuepuka mashtaka ya kufadhili vikundi vya waasi katika nchi jirani ya Sierra Leone, huku marais wawili ambao walitumikia kabla ya Taylor waliuawa.

Matukio ya kutisha ya miongo saba iliyopita nchini Liberia, ambako wastani wa watu 250,000 waliuawa wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe kati ya mwaka 1989-2003,yanamaanisha kuwa makabidhiano ya madaraka kidemokrasia hayajafanyika tangu mwaka 1944.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.