Pata taarifa kuu
ZIMBABWE-ZANU-SIASA

Mugabe asafiri kwenda Singapore kwa matibabu

Rais wa zamani wa Zimbabwe Robert Mugabe amesafiri kwa mara ya kwanza tangu kujiuzulu kwenye wadhifa wake wiki tatu zilizopita baada ya chama chake cha Zanu-PF na jeshi kumtaka afanye hivyo.

Robert Mugabe akisherehekea siku yake ya kuzaliwa, Februari 2015
Robert Mugabe akisherehekea siku yake ya kuzaliwa, Februari 2015 REUTERS/P. Bulawayo
Matangazo ya kibiashara

Mugabe ameandama na mkewe Grace Mugabe wakisafiri kwa ndege ya shirika la serikali la Air Zimbabwe kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters likinukuu maafisa kadhaa wa usalama wa Zimbabwe.

Mugabe anasafiri wakati ambapo chama chake cha Zanu-PF kinaandaa kuanzia leo Jumanne Mkutano wake mkuu ambapo siku ya Ijumaa rais mpya wa nchi hiyo Emmerson Mnangagwa atateuliwa rasmi kupeperusha bendera ya chama hicho katika uchaguzi wa urais ujao na kuteuliwa kuwa kiongozi mkuu wa chama hicho tawala tangu nchi hiyo kupata uhuru wake mnamo mwaka 1980.

Kwa mujibu wa maafisa wa Usalama walioongea na shirika la habari la Reuters, Robert Mugabe angelisafiri kwenda Singapore tarehe 16 Novemba lakini hakuweza kusafiri baada ya kuzuiliwa na jeshi nyumbani kwake siku iliyotangulia.

Mugabe alilazimika kujiuzulu baada ya kupata shinikizo kutoka kwa jeshi na maafisa wakuu wa chama chake cha Zanu-PF, baada ya kuongoza chama hicho kwa miaka 37. Jeshi lilimtaka ajiuzulu baada ya kutokea malumbani kati yake na makamu wake ambaye ni rais wa sasa Emmerson Mnangagwa, aliefutwa kazi na kukimbilia uhamishoni, kabla ya kurejea nchini kuchukua nafasi ya mtangulizi wake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.