Pata taarifa kuu

Rais mpya wa Zimbabwe awateua maafisa wa jeshi kuwa mawaziri

Siku tatu baada ya kuvunja baraza la mawaziri, rais mpya wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa ametangaza baraza lake jipya la mawaziri ambalo linaundwa na maafisa wa jeshi waliochangia kumshinikiza rais Robert Mugabe kuachia ngazi

Rais mpya wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa akihutubia wananchi wake baada ya kuapishwa, Novemba 24, 2017 katika uwanja wa mpira wa Harare.
Rais mpya wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa akihutubia wananchi wake baada ya kuapishwa, Novemba 24, 2017 katika uwanja wa mpira wa Harare. REUTERS/Philimon Bulawayo
Matangazo ya kibiashara

Rais Mnangagwa amemteua afisa mkuu wa jeshi kushikilia wizara muhimu katika serikali yake.

Afisa wa ngazi ya juu katika jeshi aliyetangaza kwenye televisheni ya taifa wiki nne zilizopita kwamba jeshi limechukua udhibiti, Jenerali Sibusiso Moyo Waziri wa Mambo ya nje.

Nae Mkuu wa jeshi la angani Perence Shiri atashikilia wizara wa ardhi.

Mnangagwa ambaye aliapishwa siku ya Ijumaa Novemba 24, aliwahutubia wananchi wake, huku akiwataka kudumisha demokrasia.

Hata hivyo, Waziri wa zamani katika serikali ya Robert Mugabe Patrick Chinamas ameteuliwa kuwa Waziri wa fedha.

Serikali ya rais huyo mpya haijawashirikisha wansiasa wa upinzani kama ambavyo ilitarajiwa.

Bw Mnangagwa alichukua hatamu ya uongozi wa Zimbabwe siku chache baada ya mtangulizi wake Robert Gabriel Mugabe kuachia ngazi kwa shinikizo la jeshi na chama chake kufuatia malumbano ndani ya chama chake kuhusu nani atakaemrithi.

Bw Mugabe alimfuta kazi makamu wake Emmerson Mnangagwa kwa kile mkewe Grace Mugabe alichokitaja kuwa alikua na njama za kutaka kumpindua mumewe katika uongozi wa nchi, madai ambayo Bw Mnangagwa alifutilia mbali na kusema ni uongo mtupu

Robert Mugabe ambaye alijiuzulu kwenye uongozi wa nchi ya Zimbabwe akiwa na umri wa miaka 93 atakua akilipwa mshahara wa dola 150,000 kila mwezi huku mkewe Grace Mugabe akilipwa nusu ya hizo, yaani dola 75,000. Mugabe vile vile amekubaliwa kupewa kiinua mgongo cha milioni 10,000,000, kwa mujibu wa gazeti la Guardian.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.