Pata taarifa kuu
DRC-AJALI

Ajali ya treni ya mizigo yaua zaidi ya watu 30 Lualaba, DRC

Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, ajali ya treni ya mizigo iliua azaidi ya watu 30 siku ya Jumapili asubuhi, 12 Novemba, katika mkoa wa Lualaba kusini mwa nchi hiyo. Watu kadhaa miongoni mwa abiria haramu walijeruhiwa katika ajali hiyo.

Ajali ya treni ya mizigo ilitokea karibu na Lubudi (ishara ya wekundu kwenye ramani), katika jimbo la Lualaba, Novemba 12, 2017.
Ajali ya treni ya mizigo ilitokea karibu na Lubudi (ishara ya wekundu kwenye ramani), katika jimbo la Lualaba, Novemba 12, 2017. Google Maps
Matangazo ya kibiashara

“Hii ni ajali mbaya kabisa kuwahi kutoka katika mkoa huu, Mkuu wa mkoa wa Lualaba, Richard Muyej, ” alisema.

Awali Bw. Muyej ameambia vyombo vya habari kwamba haijulikani ni watu wangapi waliofariki.

"Ajali hiyo ilitokea mapema Jumapili asubuhi katika kijiji kimoja kilomita 25 kutoka mji wa Lubudi, kuelekea Luena. Treni hiyo ilitupa njia na kutoakana na kuwa ilikuwa imebebea pipa za mafutaya gari, hali hiyo ilisababisha moto mkubwa, "Gavana Richard Muyej ameiambia RFI.

"Mpaka sasa kumepatikana zaidi ya miili thelathini, watu 26 waliojeruhiwa ambao walisafirishwa hospitali ya Lubudi ... Zoezi liliendelea hadi usiku. Hii ni ajali mbaya kabisa, " Richard Muyej ameongeza.

Kuhusu chanzo cha ajali hiyo, Bw Muyej anatarajia kutoa maelezo zaidi Jumatatu hii.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.