Pata taarifa kuu
SOMALIA-AL SHABAB-USALAMA

Malori ya mizigo na mafuta yapigwa marufuku Mogadishu

Serikali ya Somalia imepiga marufuku malori ya mizigo na yale ya mafuta mjini Mogadishu, wiki mbili ya mashambulizi mawili yaliyosababisha mamia ya watu.

Shambulio la kigaidi lililogharimu maisha ya watu 300 Mogadishu, mji mkuu wa Somalia, Oktoba 14, 2017.
Shambulio la kigaidi lililogharimu maisha ya watu 300 Mogadishu, mji mkuu wa Somalia, Oktoba 14, 2017. REUTERS/Feisal Omar
Matangazo ya kibiashara

Serikali hiyo imesema lengo ni kuimarisha usalama katika mji huo.

Marufuku hiyo ni kuanzia saa moja asubuhi hadi saa mbili usiku na yeyote atakayekeuka agizo, atatozwa Dola 1,000.

Somalia hivi karibuni ilikumbwa na mashambulizi mabaya kabisa kuwahi kutoka nchini humo tangu kuzuka kwa vita vya Al Shabab miaka zaidi ya 10 iliyopita.

Mashambulizi ya Al Shabab yamegharimu maisha ya watu wengi na wengine wengi kulazimika kuyahama makazi yao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.