Pata taarifa kuu
TOGO-MAANDAMANO-USALAMA

Upinzani kutoandamana wiki hii nchini Togo

Nchini Togo, upinzani unaendelea na harakati zake. Baada ya maandamano wiki iliyopita, upinzani umetoa wito wa kusalia nyumbani siku ya Ijumaa, siku ambayo wameita " Togo kufariki Ijumaa".

Togo yaendelea kukabiliwa na maandamano ya upinzani.
Togo yaendelea kukabiliwa na maandamano ya upinzani. Anne Cantener/RFI
Matangazo ya kibiashara

Wanasiasa wa upinzani aanaamini kwamba marekebisho yaliyopendekezwa na serikali hayatoshi. Mapendekezo hayo ni pamoja na ukomo wa mihula miwili kwa rais na uchaguzi utakao kuwa na duru mbili. Upinzani unasema mapendekezo hayo hayatoshina unadai kurudi kwa Katiba ya mwaka 1992 na kuondoka kwa rais wa nchi hiyo.

Kinyume na yale yaliyokua yalipangwa awali, upinzani hautoandamana wiki hii. Upinzani umepanga wiki hii kutoa heshima zao za mwisho kwa waathirika wa maandamano ya wiki iliyopita. Watu wasiopungua wanne waliuawa siku ya Jumatano iliyopita na Alhamisi wakati wa maandamano. Mtoto mmoja aliuawa kwa kupigwa risasi katika eneo la Mango, kaskazini mwa nchi, na vijana wawili walikufa maji baada ya kukimbia wakihofiwa kukamatwa na polisi walipokua katika maandamano. Upinzani unasema kuwa walikuwa wakijaribu kukimbia ukandamizaji wa polisi. Mamlaka inasema wanasubiri matokeo ya uchunguzi. Mhasiriwa wa nne ni kijana aliyepigwa risasi katika mji wa Bafilo.

Viongozi wa upinzani wamepanga kuzuru maeneo haya kukutana na familia na watu waliojeruhiwa. Tikpi Atchadam, kiongozi wa chama cha PNP, hatoaongozana na wenzake. Hajaonekana hadharani kwa muda wa zaidi ya wiki mbili, hata katika maandamano ya siku ya Jumatano na Alhamisi iliyopita, anabaini kwamba anahofia usalama wake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.