Pata taarifa kuu
LIBYA-USALAMA

Mapigano yaendelea kurindima Libya

Wanajeshi wa serikali ya libya inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa, wamekuwa wakipambana na vikosi vya waasi katka jimbo la Garabulli, Mashariki mwa jiji kuu Tripoli.

Kanali Ahmad al-Mismari, Msemaji wa jeshi la taifa la Libya.
Kanali Ahmad al-Mismari, Msemaji wa jeshi la taifa la Libya. Wikimedia commons/Reuters
Matangazo ya kibiashara

Walioshuhudia makabiliano haya wanasema wapiganaji wa waasi wanamuunga mkono aliyekuwa Waziri Mkuu Khalifa Ghweil ambaye amekataa kuitambua serikali ya Tripoli.

Umoja wa Matafa umelaani mashambulizi ya waasi hao na kusema ni lengo lao lilikuwa ni kuharibu amani na usalama ambao umekuwa ukirejea jijini Tripoli.

Wiki iliopita, Khalifa Haftar anaendesha harakati za alitangaza kwamba wapiganaji wake waliukomboa mji wa Benghazi kutoka makundi ya wanamgambo wa kiislamu na kijihadi.

Operesheni hii iliyozinduliwa katika majira ya baridi mwaka 2014, ingelidumu muda wa wiki chache, lakini ilidumu kwa zaidi ya miaka mitatu, wakati ambapo wapiganaji 5,200 wa kiongozi huyo waliuawa. Khalifa Haftar anadai kwamba jeshi lake ni la taifa ya Libya. Ushindi huu wa muda mrefu na mgumu, unampelekea Haftar kuonekana kama mtu mwenye nguvu nchini Libya.

Vikosi vya Haftar vinapambana dhidi ya muungano wa magaidi wanaunga mkono kundi la Islamic State, al-Qaeda na Ansar al-Sharia, lakini pia makundi ya kiislamu yasiyo ya kijihadi yanayompinga afisa huyo wa zamani wa ngazi ya juu katika jeshi la zamani la Mouammar Kadhafi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.