Pata taarifa kuu
SOMALIA-USALAMA

Watu sita waangamia katika shambulio Mogadishu

Watu sita wamepoteza maisha katika mlipuko wa bomu lililotokea katika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu, na wengine 10 wamejeruhiwa, kwa mujibu wa vyanzo vya usalama.

Watu waliojeruhiwa wasafirishwa hospitali baada ya mlipuko Mogadishu, Julai 30, 2017.
Watu waliojeruhiwa wasafirishwa hospitali baada ya mlipuko Mogadishu, Julai 30, 2017. REUTERS/Feisal Omar
Matangazo ya kibiashara

Bomu la lililotegwa katika gari lililipuka nje ya maduka katika mtaa wenye shughuli nyingi katika mji wa Mogadishu.

Wakati huo huo wapiganaji wa Al Shabaab wanasema wamewaua askari wengi wa kikosi cha Umoja wa Afrika AMISOM kusini mwa Mogadishu.

Lakini Msemaji wa kikosi cha askari wa Umoja wa Afrika (AMISOM) amethibitisha kuwepo kwa mapigano lakini hajasema ni wanajeshi wangapi wameuawa au kujeruhiwa katika mapigano hayo.

Usalama unaendelea kuzorota nchini Somalia kufuatia mashambulizi ya hapa na pale ya kundi la Al Shabab.

Gari dogo liliteketea kwa moto katika eneo la mlipuko,  Mogadishu , Julai 30, 2017.
Gari dogo liliteketea kwa moto katika eneo la mlipuko, Mogadishu , Julai 30, 2017. REUTERS/Feisal Omar

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.