Pata taarifa kuu
SOMALIA-UGAIDI

Serikali ya Somalia yawaonya wafanyabiashara wanaolipa kodi kwa Al Shabab

Serikali ya Somalia imetangaza kuzuia mali za wafanyabiashara wanaotoa fedha kwa kundi la kigaidi la Al Shabab.

Mji wa Mogadishu nchini Somalia
Mji wa Mogadishu nchini Somalia Open access/JamesA
Matangazo ya kibiashara

Mogadishu imesema kuwa, imebaini kuwa kundi la Al Shabab limekuwa likichukua fedha kama kodi kutoka kwa baadhi ya wafanyabiashara katika maeneo wanayodhibiti.

Waziri Mkuu Hassan Ali Kheyre amewashutumu baadhi ya wafanyabiashara nchini humo kulipa fedha kwa wanamgambo wa Al Shabab badala ya kufanya hivyo kwa serikali.

Kampuni zilizolengwa hasa ni zile za mawasiliano lakini pia zile zinapokea fedha kutoka kwa raia wa nchi hiyo wanaoishi nje ya nchi.

Waziri wa usalama Mohamed Abukar Islow ameonya kuwa ikiwa wafanyabiahsara hao hawatabadilika, watafungiwa na kutiwa mbarani.

Hatua kubwa ya kutofanikiwa kulimaliza kundi hili ni kutokana na kuendelea kupata fedha zinazowasaidia katika harakati zao ikiwa ni pamoja na kununua silaha.

Al Shabab linasalia kundi hatari kwa usalama wa serikali ya Somalia na hata katika nchi jirani ya Kenya na Ethiopia.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.