Pata taarifa kuu
LIBYA-UN-USALAMA

Ghassan Salame ateuliwa mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini Libya

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa liliidhinisha Jumanne Juni 20 uteuzi wa Mjumbe Maalum wa Umoja huo nchini Libya. Bw Salame aliteuliwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres.

Ghassan Salame hapa ni katika mwaka 2012.
Ghassan Salame hapa ni katika mwaka 2012. wikimedia cc
Matangazo ya kibiashara

Baada ya kuongezwa miezi minne kwa Martin Kobler mjumbe wa sasa wa Umoja wa Mataifa nchini Libya kutokana na ukosefu wa makubaliano juu ya watu waliopendekezwa kwenye kwa nafasi hii, uteuzi wa mpatanishi wa kimataifa na aliyekuwa Waziri wa Utamaduni wa Libanon Ghassan salame Lebanon ulifanyika kwa makubaliano. Kama kazi hii inaonekana ngumu, mjumbe mpya ana njia nyingi za kushughulikia suala hilo.

Bw Salame ana mahusiano ya kirafiki na wanasiasa wengi nchini Libya na nchi za Ghuba, nchi zenye ushawishi katika kesi ya Libya, kama vile Qatar, Saudi Arabia na Milki za Kiarabu.

Uzoefu wake wa kimataifa humpa faida ya ziada. Alikuwa mshauri wa aliyekuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan. Katika muktadha huu, alifanya kazi nyingi za Umoja wa Mataifa nchini raq na Burma.

Ghassan salame pia ni rafiki wa karibu wa Katibu Mkuu wa sasa wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.