Pata taarifa kuu
AFRIKA KUSINI

Zuma asema ubaguzi wa rangi nchini mwake unashuhudiwa wazi

Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma amesema maandamano ya maeflu ya watu yaliyofanyika kote nchini humo kutaka ajiuzulu, ni ushahidi tosha kuwa nchi hiyo inaendelea kukabiliwa na ubaguzi wa rangi.

Rais wa Afrika Kusini  Jacob Zuma
Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma Reuters/Rogan Ward
Matangazo ya kibiashara

Zuma ametoa matamshi haya siku ya Jumatatu katika maadhimisho ya miaka 24 kumkumbuka mwanaharakati wa vita wa ubaguzi wa rangi nchini humo na aliyekuwa kiongozi wa chama cha Kikomunisti Chris Hani.

Shinikizo hizi zinakuja baada ya rais Zuma, wiki iliyompita kumfuta kazi Waziri wake wa fedha Pravin Gordhan.

Maandamano hayo yamefanyika katika miji ya Pretoria, Johannesburg na Cape Town wakiimba na kusema wamechoka na uongozi wa Zuma kwa sababu za ufisadi na uongozi mbaya.

Licha ya shinikizo hizi, uongozi wa juu wa chama tawala ANC umemtetea rais Zuma na kusema hakuna haja na ushahidi wa kumlazimisha Zuma kujiuzulu.

Mbali na maandamano haya, wabunge wa chama cha upinzani wamesema kuwa watawasilisha mswada wa kukosa imani na rais Zuma kwa madai ya ufisadi.

Wanaompinga rais Zuma wanasema alimfuta kazi Waziri Gordhan kwa sababu amekuwa katika mstari wa mbele kupambana na ufisadi, huku wanaomuunga mkono wakisema wanaridhika na mabadiliko aliyoyafanya pamoja na uongozi wake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.