Pata taarifa kuu
AFRIKA KUSINI

Chama cha ANC chagawanyika baada ya kufutwa kazi kwa Gordhan

Hatua ya rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma kumfuta kazi Waziri wa Fedha Pravin Gordhan, imesababisha mgawanyiko katika chama tawala ANC.

Aliyekuwa Waziri wa fedha nchini Afrika Kusini  Pravin Gordhan
Aliyekuwa Waziri wa fedha nchini Afrika Kusini Pravin Gordhan REUTERS/Siphiwe Sibeko
Matangazo ya kibiashara

Mbali na mgawanyiko huo, thamani ya Rand imeshuka.

Makamu wa rais Cyril Ramaphosa, ambaye anaonekana kama mmoja wa watu wanaopewa nafasi kubwa ya kumrithi rais Zuma, amesema hatua ya kufutwa kazi kwa Gordhan haikubaliki.

Matamshi ya Ramaphosa, ambaye siku zote amekuwa akionekana kumuunga mkono Zuma, yanaonesha wazi mgawanyiko ndani ya chama hicho tawala.

Hata hivyo, vuguvugu la wanawake na vijana katika chama hicho, kwa pamoja yameunga mkono mabadiliko hayo na kusema ni ya manufaa kwa watu weusi nchini humo.

Vyama vya upinzani navyo vimelaani hatua hii na kudai, Gordhan alikuwa katika mstari wa mbele kupambana na ufisadi na kuwazuia washirika wa rais Zuma kuiba fedha za umma.

Hata hivyo, Zuma na wafuasi wake wamekuwa wakimshutumu Waziri huyo wa zamani kuhusika na maswala ya ufisadi kwa kushirikiana na Familia ya matajiri wa Kihindi ya Guptas.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.