Pata taarifa kuu
SWAZILAND-UKRISTO

Swaziland: Shule kufundisha Ukristo

Katika taarifa iliyotumwa kwa wakuu wote wa shule nchini Swaziland, Wizara ya Elimu imeamuru kufuta programu za dini ya Uislamu. Swaziland  ni nchi yenye Wakristo wengi licha ya kuwepo kwa dini nyingine. 

Mfalme Mswati III akilihutubia taifa katika uwanja wa Somhlolo, Septemba 6, 2010 Swaziland.
Mfalme Mswati III akilihutubia taifa katika uwanja wa Somhlolo, Septemba 6, 2010 Swaziland. /AFP PABALLO THEKISO
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa serikali ya Swaziland, uamuzi huu umechukuliwa kwa minajili ya kuepuka kuwachanganya wanafunzi wa wa Swaziland.

Uamuzi huu unakuja baada ya kuundwa mwaka jana kwa tume ya uchunguzi ya bunge kufuatia malalamiko kuhusu ushawishi wa wahamiaji wa Kiislamu.

Swaziland, ni nchi yenye Wakristo wengi

Katiba ya Swaziland inatambua uhuru wa dini na kuabudu, licha ya kuwaUkristo unongoza nchini humo.

Hata hivyo nchi hii ina dini nyingine. Waislamu ni 2%, kulingana na ripoti ya Idara ya Marekani kuhusu uhuru wa dini duniani iliyochapishwa mwaka 2015.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.