Pata taarifa kuu
MAREKANI-SUDAN

Marekani yaongeza muda wa vikwazo kwa nchi ya Sudan

Rais wa Marekani, Barack Obama, ameongeza muda wa vikwazo kwa nchi ya Sudan kwa mwaka mmoja zaidi, akisema kuwa sera za utawala wa Khartoum bado zimeendelea kuwa tishio kwa usalama wa Marekani.

Rais wa Marekani, Barack Obama.
Rais wa Marekani, Barack Obama. REUTERS/Jonathan Ernst
Matangazo ya kibiashara

Nchi ya Sudan imewekewa vikwazo vya kibiashara na Serikali ya Marekani toka mwaka 1997, ikituhumiwa kwa kuyaunga mkono makundi ya wapiganaji wa Kiislamu.

Aliyekuwa kiongozi wa mtandao wa kigaidi duniani wa Al-Qaeda, Osama bin Laden alikuwa amepiga kambi jijini Khartoum kuanzia mwaka 1992 hadi 1996.

Hata hivyo hivi karibuni utawala wa Khartoum umekuwa ukituhumiwa kutekeleza mauaji ya halaiki dhidi ya raia wanaoishi kwenye jimbo la Darfur, hatua ambayo huenda ikawa imeishawishi nchi ya Marekani kuongeza muda wa vikwazo.

Jumatatu ya wiki hii, Rais Obama ametangaza kuongezwa kwa muda wa mwaka mmoja zaidi kwa utawala wa Khartoum, kuanzia November 3 mwaka huu.

Awali kulikuwa na taarifa kuwa huenda nchi ya Marekani ingelegeza baadhi ya vikwazo vyake kwa nchi ya Sudan, hasa baada ya ziara kadhaa zilizofanywa hivi karibuni nchini humo na mjumbe maalumu wa Marekani, Donald Booth.

Rais wa Sudan, Omar al-Bashir, picha imepigwa October 30, 2016.
Rais wa Sudan, Omar al-Bashir, picha imepigwa October 30, 2016. REUTERS/Mohamed Nureldin Abdallah

Kwenye taarifa yake kwa uma, ubalozi wa Marekani jijini Khartoum umesema kuwa, uamuzi wa kuongezwa kwa mwaka mmoja zaidi, ni uamuzi uliochukuliwa kwa sababu za kifundi zaidi na kwamba haimanishi kuwa baadhi ya vikwazo vinaweza kulegezwa.

Marekani ambayo iliiorodhesha nchi ya Sudan kama taifa linalofadhili ugaidi duniani toka mwaka 1993, imesema itaendelea kuzungumza na Sudan kuhusu uwezekano wa kubadili baadhi ya sera zake.

Utawala wa Washington ulikuwa muumini mkubwa wa kujitenga kwa nchi ya Sudan Kusini kutoka Sudan mwaka 2011, hatua ambayo wengi waliiona kuwa huenda Marekani ingelegeza vikwazo vyake kama zawadi.

Hata hivyo machafuko kwenye jimbo la Darfur yameendelea kusababisha sintofahamu katika uhusiano wa nchi hizo mbili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.