Pata taarifa kuu
SUDAN-MAREKANI

Marekani yatia ngumu kuuondolea vikwazo utawala wa Khartoum

Wizara ya mambo ya nje ya Marekani, imeipongeza Serikali ya Sudan, Khartoum kwa juhudi zake za kupambana na vitendo vya kigaidi, lakini ikakataa kuiondolea vikwazo nchi hiyo iliyoko kwenye pembe ya Afrika Mashariki.

Rais wa sudan, Omar Al Bashir, akiwasili Khartoum, Juni 15 mwaka 2015, akitokea Johannesburg.
Rais wa sudan, Omar Al Bashir, akiwasili Khartoum, Juni 15 mwaka 2015, akitokea Johannesburg. REUTERS/Mohamed Nureldin Abdallah
Matangazo ya kibiashara

Marekani inasisitiza kuwa vikwazo hivi vitaendelea kuwepo hadi pale hali ya amani na utulivu itakaporejea kwenye jimbo la Darfur, ambapo imetoa wito kwa Serikali kukubali na kuheshimu uwepo wa vikosi vya walinda amani kwenye eneo hilo.

Serikali ya Sudan imewekewa vikwazo vya kiuchumi na biashara na nchi ya Marekani toka mwaka 1997 ikidaiwa kuwa ilikuwa na uhusiano na makundi ya kigaidi.

Hata hivyo mwaka 2007 utawala wa iliyokuwa Serikali ya Rais Bush, ilitangaza kuiwekea nchi hiyo vikwazo vipya, kwa kile ilichodai kuwa ni kuhusika kwake na vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu kwenye jimbo la Darfur.

Mwezi Juni pia mwaka 2012, mjumbe maalumu wa Marekani Princeton Lyman, alisema kuwa, kuhusishwa kwa Rais Bashir na makosa ya uhalifu wa kivita pamoja na kutolewa kwa hati ya kukamatwa kwake na mahakama ya kimataifa ya ICC, kunafanya ugumu zaidi kwa vikwazo hivyo kuondolewa.

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani, John Kirby, amesema kuwa licha ya kupongeza hatua kubwa iliyopigwa na utawala wa Khartoum kwenye vita dhid ya ugaidi, wao wanaona kuwa bado Serikali haijafanya vya kutosha katika kushughulikia mzozo wa Darfur.

Kauli ya Marekani imekuja ikiwa ni siku chache zimepita, ambapo maofisa wa Serikali ya Sudan walikuwa nchini humo kuzungumza na utawala wa Rais Obama, kuangalia uwezekano wa nchi hiyo kuiondolea vikwazo, ushawishi ambao hata hivyo unaonekana haujafua dafu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.