Pata taarifa kuu
BOTSWANA-ICC

Waziri wa mambo ya nje wa Botswana, apinga nchi za Afrika kujitoa ICC

Nchi kadhaa za Afrika zimejitokeza kupinga waziwazi uamuzi unaochukuliwa na baadhi ya wanachama wenzao ndani ya umoja wa Afrika, kutangaza kujitoa kwenye mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ya ICC.

Nkosazana Dlamini-Zuma, mkuu wa tume ya umoja wa Afrika, AU.
Nkosazana Dlamini-Zuma, mkuu wa tume ya umoja wa Afrika, AU. REUTERS/Tiksa Negeri
Matangazo ya kibiashara

Safari hii waziri wa mambo ya nje wa Botswana, Pelomoni Venson-Moitoi ambaye pia anawania nafasi ya kuteuliwa kuwa mkuu mpya wa tume ya umoja wa Afrika, amekosoa uamuzi uliochukuliwa na baadhi ya nchi kujitoa kwenye mahakama hiyo.

Venson-Moitoi anasema kuwa nchi hizo na nchi nyingine za Afrika, badala ya kujitoa kwenye mahakama ya ICC, zinapaswa kuketi na kufanya mabadiliko ambayo wanataka kuyaona ndani ya mahakama hiyo.

Wakati huu nchi wanachama za umoja wa Afrika zikiendelea kuweka shinikizo kwenye mahakama kujitoa, Venson-Moitoi anayataka mataifa hayo ikiwemo Afrika Kusini, kufanya ushawishi wa mahakama ya Afrika kufanya kazi pamoja na mahakama hiyo.

“Sioni kwanini tujitoe. Kitu kizuri ni kuwa wanachama wachache wa ICC, wanakubaliana kimsingi kuwa hakuna haja ya nchi za Afrika kujiondoa kwa sababu sio suluhu ya tatizo. Tunapaswa kufanya kazi pamoja kutatua tatizo sio kuongeza tatizo”. Alisema Venson-Moitoi.

Saa chache baada ya matamshi yake, nchi ya Gambia nayo imetangaza kujiondoa kwenye mahakama ya ICC, ikiituhumu mahakama hiyo kwakuwa na upendeleo na kuwalenga viongozi wa Afrika peke yake.

Hata hivyo Venson-Moitoi huenda asiipate nafasi hiyo kutokana na matamshi yake haya, kwakuwa mpinzani wake wa karibu ni waziri wa mambo ya nje wa Kenya, Amina Mohamed, ambaye anaunga mkono nchi za Afrika kujiondoa kwenye mahakama ya ICC.

Uchaguzi wa kumpata mrithi wa Nkosazana Dlamini-Zuma, unatarajiwa kufanyika mwezi January mwakani wakati wa mkutano wa wakuu wa nchi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.