Pata taarifa kuu
DRC-USALAMA

FARDC yawaua waasi wanne wa FDLR katika mji wa Rutshuru

Majeshi ya DRC (FARDC) yamewaua kwa risasi wapiganaji wanne wa kundi la waasi wa Kihutu wa Rwanda la FDLR na kuwakamata wengine wawili wakati wa shambulizi lilofanywa Jumapili hii Oktoba 23 mjini Rutshuru, mkoani Kivu Kaskazini. Jeshi la DR Congo pia limekamata silaha tano za kivita kutoka mikononi mwa waasi hao wa Rwanda.

Vikosi vya jeshi la DR Congo (FARDC) mjini  Kibati, karibu na mji wa Goma.
Vikosi vya jeshi la DR Congo (FARDC) mjini Kibati, karibu na mji wa Goma. REUTERS/Thomas Mukoya
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa mjumbe rasmi katika mji wa Kiwanja, yote yalianza baada ya askari kumkamata Jumamosi iliyopita, kijana mmoja, mfanyabiashara, anayetuhumiwa na wakazi wa mji huo kushirikiana na FDLR.

Baada ya kufanya msako katika nyumba ya mfanyabiashara huyo, askari walimkuta mpiganaji mmoja wa kundi la waasi la FDLR.

Kwa mujibu wa redio Okapi, kijana huyo baadaye alikiri kushirikiana na waasi hao wa Rwanda ambao alikua akiwapa hifadhi mara kwa mara nyumbani kwake wakati wanapokua na kazi ya upelelezi katika mji wa Rutshuru.

Baada ya mpiganaji huyo wa FDLR kukamatwa, kijana huyo mfanyabiashara alitakiwa kwenda kuonyesha kambi ya waasi hao. Wakati huo jeshi la FARDC lilivamia ngome moja ya waasi hao. Jeshi lilifaulu kuwaua wapiganaji wanne wa FDLR na kuwakamata wengine wawili. Waasi wengine waliweza kutimka.

Kwa sasa, kijana huyo mfanyabiashara aliyekua akiwapa hifadhi waasi hao waRwanda anazuiliwa katika gereza la Nyongera mjini Kiwanja.

Mwezi Juni, jeshi pia lilifaulu kuvunja ngome ya waasi wa kundi la FDLR katika kijiji cha Kazaroho wilayani Rutshuru mkoani Kivu Kaskazini.

Kwa mujibu wa msemaji wa operesheni Sokola 2, Kapteni Njike Kaiko, ngome hiyo ya waasi ilivunjwa katika operesheni iliyoendeshwa na Jeshi la DR Congo (FARDC) likisaidiwa na kikosi cha Umoja wa Mataifa chni Dr Congo (MONUSCO).

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.