Pata taarifa kuu
LLIBYA-ITALIA-WAHAMIAJI

Wahamiaji 5,600 waokolewa kwenye pwani ya Libya

Jumatatu wiki hii, Oktoba 3, vikosi vya majini nchini Italia viliwaokoa wahamiaji zaidi 5,600 kwenye pwani ya Libya katika bahari ya Mediterania. Watu hao waliokolewa na meli kadhaazilizotumwa katika bahari ya Mediterania. Meli ya shirika lisilo la kiserikali la SOS Mediterranean ni miongoni mwa meli hizo.

Katika bahari ya Mediterrania, kwenye umbali wa maili 20 na pwani ya Libya, wahamiaji wakisubiri Jumatatu hii, Oktoba 3, 2016, kuokolewa.
Katika bahari ya Mediterrania, kwenye umbali wa maili 20 na pwani ya Libya, wahamiaji wakisubiri Jumatatu hii, Oktoba 3, 2016, kuokolewa. ARIS MESSINIS / AFP
Matangazo ya kibiashara

Vikosi vya majini nchini Italia vimesema zaidi ya wahamiaji elfu sita waliokuwa wakijaribu kuingia barani ulaya wameokolewa maji hapo jana.

Maiti tisini zimeweza kupatikana na miongoni mwa maiti hizo ni ya mwanamke mjamzito mwenye umri wa miaka ishirini na tatu.

Vikosi hivyo vinavyoshika doria katika fukwe ya bahari ya Mediterania nchini Italy wamesema zaidi ya watu mia saba walikuwa wamepanda katika boti hiyo na watoto wapatao mia mbili.

Kwenye pwani ya Libya, Jumatatau wiki hii kulifanyika operesheni kumi na mbili za uokoaji, kwa mujibu wa vikosi vya majini vya Italia. Wahamiaji hao walikua wakielekea barani ulaya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.