Pata taarifa kuu
MISRI-AJALI

Wahamiaji zaidi ya 42 wafariki baada ya boti kuzama katika Bahari ya Mediterranean

Kwa uchache watu 42 walifariki Jumatano baada ya kuzama kwa boti ya wahamiaji katika Bahari ya Mediterranean, karibu na pwani ya MisriBoti hiyo iliku imebeba watu takriban 450 kwa mujibu wa ushahidi uliyotolewa na watano miongoni mwa walionusurika. Boli hili lilizama karibu na mji wa Rosette, mji wa wenye bandari katika eneo la Delta Nile. 

Watu wa kujitolea wanajipanga kufanya shughuli ya uokozi wakati ambapo boti lililobeba wakimbizi kijiandaa kutua kwenye bandari ya kisiwa cha Lesbos, Otoba 2,2015.
Watu wa kujitolea wanajipanga kufanya shughuli ya uokozi wakati ambapo boti lililobeba wakimbizi kijiandaa kutua kwenye bandari ya kisiwa cha Lesbos, Otoba 2,2015. REUTERS/Dimitris Michalakis
Matangazo ya kibiashara

Shughuli za uokoaji zimekua zikiendelea Jumatano usiku ili kupata abiria wengine waliokua wakisafiri na boti hiyo ya wahamiaji ambayo ilikwama karibu na eneo la Rosetta, katika pwani ya kaskazini ya Misri, maafisa wa polisi wameliambia shirika la habari la AFP.

Wahamiaji kutoka "Misri, Sudan na mataifa mengine ya Afrika ambayo hayajaweza kutajwa ni miongoni mwa wahanga," Adel Khalifa, afisa kutoka Wizara ya Afya ya Misri ameliambia shirika la habari la AFP.

"Watu 29 wamefariki na wengine watano kujeruhiwa baada ya boti llililokua likisafirisha wahamiaji haramu kuzama", Wizara ya Afya imebaini katika taarifa yake, huku ikiongeza kuwa magari 15 ya wagonjwa yametumwa katika eneo la tukio ili kusaidia waathirika.

Ripoti ya awali ya wizara ilibaini watu10 wamefariki katika ajali hiyo.

Tangu mwanzoni mwa majira ya joto, kuliongezeka idadi kubwa ya boti za uvuvi zilizokua zikitokea katika pwani ya kaskazini ya Misri na mamia ya watu ziliokolewa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.