Pata taarifa kuu
NILE

Ethiopia, Misri na Sudan kufanya utafiti kuhusu ujenzi wa bwawa la umeme kutumia maji ya mto Nile

Nchi za Misri, Sudan na Ethiopia zimekubaliana na kutoa kibali cha kufanyika kwa utafiti wa kitaalamu wa kimazingira na kiuchumi kuangalia athari zinazoweza kujitokeza kutokana na ujenzi wa bwawa kubwa la kuzalisha umeme linalotaka kujengwa na nchi ya Ethiopia ikitumia maji ya mto Nile.

Picha ikionesha ujenzi wa bwawa kubwa la kuzalisha umeme nchini Ethiopia ukiendelea, nchi za Sudan, Misri na Ethiopia zimekubaliana kufanyika kwa utafiti wa athari za kiuchumi na kimazingira.
Picha ikionesha ujenzi wa bwawa kubwa la kuzalisha umeme nchini Ethiopia ukiendelea, nchi za Sudan, Misri na Ethiopia zimekubaliana kufanyika kwa utafiti wa athari za kiuchumi na kimazingira. Ethiopia govt
Matangazo ya kibiashara

Bwawa hilo ambalo litaigharimu nchik ya Ethiopia kiasi cha dola za Marekani bilioni 4, linatarajiwa kuwa bwawa kubwa zaidi barani Afrika ambalo litashuhudia nchi ya Ethiopia ikiwa mzalishaji na msambazaji mkubwa wa nishatik ya umeme kwenye bara hilo.

Bwawa hilo ambalo litakuwa na uwezo wa kuzalisha megawati zaidi ya elfu 6, litajengwa jirani kabisa na mpaka wa nchi hiyo na Sudan na linajengwa na kampuni ya kiitaliano Salin Impregilo na linatarajiwa kukamilika mwaka ujao.

Bwawa hilo limekuwa chanzo cha mvutano kati ya Ethiopia na Misri, ambapo utawala wa Addis Ababa unategemea kwa asilimia mia moja maji yanayotoka kwenye mto Nile ambao ni chanzo muhimu cha maji kwa nchi ya Misri.

Serikali ya Addis Ababa inautuhumu utawala wa Cairo kwa kukimbilia kwa nchi wafadhili wa mradi huo, ambazo sasa zimesitisha kwa muda msaada wake ambao utachelewesha kukamilika kwa muda wa ujenzi wa bwawa hilo, huku utawala wa Cairo wenyewe ukitaka kwanza hakikisho kuwa mtiririko wa maji ya mto Nile kwenda nchini mwake hautaathiriwa.

Taarifa iliyoyolewa na kituo cha taifa cha Misri, imesema kuwa nchi hizo tatu zimetiliana saini na kampuni huru za Ufaransa ili zifanye utafiti wa kitaalamu kuhusu athari za kimazingira na kiuchumi kuhusu ujenzi wa bwawa hilo.

Utafuti huo unatarajiwa kuanza wakati wowote kuanzia sasa na unatarajiwa kuchukua muda wa miezi 11.

Maji ya mto Nile mbali na kuwa kitovu kwa nchi hizo mbili kwa shughuli mbalimbali za kibinadamu, pia yanatumiwa na nchi za ukanda wa Afrika Mashariki ikiwemo Kenya, Uganda na Tanzania ambazo nazo zinataka kuheshimiwa kwa maji ya mto huo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.