Pata taarifa kuu
DRC-MAZUNGUMZO

Maaskofu nchini DRC wasisitiza umuhumi wa mazungumzo shirikishi

Baraza la kitaifa la Maaskofu wa kanisa katoliki nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, limesisitiza wito wake juma hili wa kuwa na mazungumzo ya kitaifa ambayo yanashirikisha pande zote na kwakuzingatia katiba ya nchi.

Baadhi ya maaskofu wa DRC ambao wamo kwenye baraza la maaskofu, aliyeko katikati ni Askofu Nicolas Djomo, mwenyekiti wa baraza hilo
Baadhi ya maaskofu wa DRC ambao wamo kwenye baraza la maaskofu, aliyeko katikati ni Askofu Nicolas Djomo, mwenyekiti wa baraza hilo Photo: Flickr/Mazur/catholicnews.org.uk/CC BY-NC-SA 2.0
Matangazo ya kibiashara

Katika taarifa yao kwa vyombo vya habari iliyotolewa Jumanne ya September 6, baraza hilo la maaskofu, linasema kuwa kamwe haliwezi kushiriki kwenye mazungumzo ya kitaifa yanayoendelea hivi sasa ikiwa masuala haya muhimu waliyoyaeleza hayakuzingatiwa.

Taarifa yao imeongeza kuwa, kwa kuwa na mazungumzo ya kweli na ya wazi ambayo yatasababisha kumalizika kwa mzozo wa kisiasa kwenye taifa hilo, baraza lao lina waalika wadau wote nchini humo ilikuwa kuwa na changanyiko shirikishi.

Baraza la Maaskofu linasema kuwa, wao wanaamini kushirikishwa kwa viongozi wa kuu na muhimu wa upinzani kwenye mazungumzo hayo, kutatoa nafasi kwa nchi hiyo kufikia malengo ya kutatua kasoro ambazo zinashuhudiwa kwa sasa.

Katika muktadha huo, CENCO imesema inaunga mkono juhudi za kijasiri zilizofanywa na Serikali kwa kuanza kuwaachia baadhi ya wafungwa wa kisiasa, na kwamba ni kwa moyo huo ndipo amani na suluhu huenda ikapatikana.

Hata hivyo maaskofu hao wametaka kuachiwa kwa wafungwa zaidi wa kisiasa bila kuwataja majina.

Maaskofu hao wameongeza kuwa, mazungumzo ni lazima yafanywe kwa kuzingatia na kuheshimu katiba ya nchi, na kusisitiza kuhusu kuheshimiwa kwa kipengele ambacho kinahusu muhula wa rais kukaa madarakani na kukabodhi madaraka kidemokrasia.

Mazungumzo haya ambayo yaliitishwa mwaka 2015 na Rais Josephu Kabula, yalifunguliwa rasmi September Mosi mwaka huu jijini Kinshasa bila ya uwepo wa viongozi wakuu wa upinzani, ambao wametoa masharti ya wao kushiriki kwenye mazungumzo hayo.

Miongoni mwa matakwa ya upinzani ni pamoja na kuachiwa huru kwa wafungwa wote wa kisiasa wanaoshikiliwa, kufutwa kwa kesi zinazowakabili baadhi ya wanasiasa na kuondolewa kwa mpatanishi aliyeko hivi sasa, waziri mkuu wa zamani wa Togo, Edem Kodjo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.