Pata taarifa kuu
DRC-MAZUNGUMZO

Ufunguzi wa mazungumzo DRC: Upinzani wasema watu kadhaa wakamatwa

Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, kulianzishwa Alhamisi hii mchana mazungumzo ya kitaifa ya uchaguzi wa amani. Walikuwepo katika sherehe hiyo wawakilishi wa Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa.

Makabiliano kati ya polisi na vijana wafuasi wa vyama vya upinzani pembezoni mwa makao makuu ya vyama vya upinzani kabla ya ufunguzi wa mazungumzo.
Makabiliano kati ya polisi na vijana wafuasi wa vyama vya upinzani pembezoni mwa makao makuu ya vyama vya upinzani kabla ya ufunguzi wa mazungumzo. RFI / Sonia Rolley
Matangazo ya kibiashara

Wakati huo huo, makabiliano yalizuka kati ya vijana wafuasi wa upinzani mkutano na vikosi vya polisi. Muungano wa vyama vya upinzani umebaini kwamba watu wengi wamekamatwa.

Viongozi wa wa upinzani walitaka kuwasilisha madai yao wakiongozana na wafuasi wao vijana katika makao makuu ya Umoja wa Afrika na MONUSCO. Msemaji wa polisi almesema hakukuwa na haja ya vijana kwa kuwasilisha waraka huo na hawakuruhusiwi kuandamana kwenye barabara kuu.

Mamia ya watu walikamatwa, kwa mujibu wa muungano wa vyama vya upinzani unaoongozwa na Etienne Tshisekedi ambapo 90 walikamatwa katika kata ya Gombe, huku polisi ikibaini kuwa watu waliokamatwa katika kata hiyo ni 85. Makabiliano yalishuhudiwa kwa masaa kadhaa. Wafuasi wa upinzani walikua wakirusha mawe, huku polisi ikitumia mabomu ya machozi. Wakati huo huo makabiliano mengine kati ya wafuasi wa vyama vya upinzani vinavyounga mkono mazungumzo na vile vinavyopinga yalishuhudiwa katika maeneo mbalimbali ya mji wa Kinshasa.

LKiongozi wa chama cha UNC, Vital Kamerhe, akihojiwa na vyombo vya habari wakati wa ufunguzi wa mazungumzo.
LKiongozi wa chama cha UNC, Vital Kamerhe, akihojiwa na vyombo vya habari wakati wa ufunguzi wa mazungumzo. RFI / Sonia Rolley

Hata hivyo wafuasi wa chama madarakani na vile vinayokiunga mkono waliandamana kwa minajili ya kuunga mkono mazungumzo kwa kuonyesa furaha yao, bila ya kuzuiliwa.

Baadhi ya vyama vya upinzani vimesema havina imani na msuluhishi W+Edem Kodjo, huku Umoja wa Afrika ukisema unamuunga mkono ili aendelee na mazungumzo kwa lengo la kupatia ufumbuzi mgogoro wa kisiasa unaoikabili nchi hiyo kwa miezi kadhaa.

Hata hivyo Eden Kojdo ameonyesha haja ya kutokua na upendeleo wowote katika majukumu yake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.