Pata taarifa kuu
CAR-MINUSCA-DRC-UBAKAJI

CAR: MINUSCA yakabiliwa na tuhuma mpya za unyanyasaji wa kijinsia

Watoto wanne wanaoishi katika kambi ya wakimbizi wa ndani nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati walidhalilishwa kijinsia na askari wa kulinda amani kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo

wanajeshi wa MINUSCA wakpiga doria karibu na  kituo cha kupigia kura mjini Bangui, baada ya uchaguzi wa urais na wawabunge, Jamhuri ya Afrika ya kati , Januari 2, 2016.
wanajeshi wa MINUSCA wakpiga doria karibu na kituo cha kupigia kura mjini Bangui, baada ya uchaguzi wa urais na wawabunge, Jamhuri ya Afrika ya kati , Januari 2, 2016. ISSOUF SANOGO / AFP
Matangazo ya kibiashara

Sifa ya askari wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa imechafuliwa katika miezi ya hivi karibuni na mfululizo wa kashfa za ngono. Jumanne hii, msemaji wa Umoja wa Mataifa amesema kuwa askari kadhaa wa kulinda amani kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) wametuhumiwa kuwadhalilisha vibaya watoto wanne wanaoishi katika kambi ya wakimbizi wa ndani nchiniJamhuri ya Afrika (CAR).

Makosa yaliotendwa kati ya mwaka 2014 na 2015

Waathirika wanne walidhalilishwa kingono kati ya mwaka 2014 na 2015. Umoja wa Mataifa ulipokea mashtaka Februari 11 kutoka mashirika yasio ya kiserikali ambayo yalitoa taarifa kwamba watoto wanne waliokuwa wakiishi katika kambi ya wakimbizi wa ndani ya Ngakobo, katika mkoa wa Ouaka nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati. Serikali ya DRC imepewa taarifa Jumatatu hii kuhusu kesi hii na ina sasa siku kumi ili kuamua kama itaendesha uchunguzi wake mwenyewe kuhusu askari wake au itapendelea kuwa Umoja wa Mataifa ujihusishe na kesi hiyo.

Mratibu maalumu aliteuliwa wiki iliyopita

Kufuatia matukio kadhaa ya madai ya unyanyasaji wa kijinsia yalioarifiwa katika Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati (MINUSCA), Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, alimfuta kazi mkuu wa Ujumbe huo mwezi Agosti mwaka 2015 na kuteua tume ya wataalam.Tume hii ilibaini kwamba bado kuna mapungufu makubwa katika mfumo mzima wa utendaji kazi wa Umoja wa Mataifa. Wiki iliyopita Umoja wa Mataifa ulimteua mratibu maalum, Jane Holl Lute, raia wa Marekani, atakaye husika na kuboresha majibu yake katika eneo hili.

Kati ya kesi 69 za kashfa ya ngono zinazoaminiwa kuorodheshwa mwaka jana na Umja wa Mataifa katika Jumbe zake 16 za kulinda amani duniani kote, kesi 22 zinahusu Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati (MINUSCA).

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.