Pata taarifa kuu
BURUNDI-MAKABURI YA HALAIKI

Burundi: mashahidi wabaini kuwepo kwa makaburi ya halaiki

Nchini Burundi, wakazi wa mji wa Bujumbura wana wasiwasi kuhusu kuwepo kwa makaburi ya halaiki kufuatia mauaji ya Desemba 11. Makambi ya kijeshi yalishambuliwa na mauaji yalifuatiwa. Msemaji wa jeshi alisema wakati huo kuwa " maadui 79 waliuawa.

Kaburi la hakaiki linaloshukiwa kuwepo katika msitu wa Rukoko karibu na makaburi yanayotambuliwa rasmi ya Mpanda ambapo mashahidi wanasema waliona maiti kumi na tano za askari na raia wa kawaida wakizikwa na polisi Desemba 11.
Kaburi la hakaiki linaloshukiwa kuwepo katika msitu wa Rukoko karibu na makaburi yanayotambuliwa rasmi ya Mpanda ambapo mashahidi wanasema waliona maiti kumi na tano za askari na raia wa kawaida wakizikwa na polisi Desemba 11. © RFI
Matangazo ya kibiashara

" Mashirika ya ndani na nje ya kutetea haki za binadamu, ikiwa ni pamoja na FIDH, yalieleza wakati huo kwamba watu zaidi ya 154 waliuawa na vijana 150 hawajulikani waliko. Familia nyingi za mji wa Bujumbura zimeendelea kulalamika kuhusu kutowapata ndugu zao.

Kwa upande wao viongozi mbalimbali, ikiwa ni pamoja na viongozi wa serikali za mitaa, wamesema hakuna jambo la kushangaza. Miili ya watu wasiojulikana kutoka Nyakabiga, Ngagara na Musaga ilizikwa Desemba 12 saa 5:00 mchana katika makaburi ya Kanyosha na Mpanda. Wote walikua washambuliaji au watu walioshirikiana nao ambao walizikwa baada ya kuuawa katika mashambulizi ya Desemba 11 dhidi ya makambi ya kijeshi, serikali imesema. Kwa ujumla watu 58 waliuawa.

Lakini kwa mtu huyo ambaye alikua akifanya kazi karibu na makaburi ya Mpanda wakati miili ya watu waliouawa ilizikwa, amesema haikua rahisi. "Watu wanaogopa kuzungumza kuhusu suala hilo kwa sababu askari polisi waliwatishia usalama wao iwapo watathubutu kuzungumza lolote kuhusu mkasa huo". Mmoja wa maafisa ambao waliambatana na wafanyakazi mbalimbali wa Idara za manispaa ya jiji katika zoezi hio amesema : "walituambia kuwa ni siri kati yetu na wakuu wa wilaya. "

Shahidi huyo amesema aliona miili 25 katika makaburi matano ambayo yako karibu na eneo wanakozikwa viongozi serikalini. Idadi hii ni sambamba na ile inayotolewa na viongozi ambao wameanza kuweka wazi mkasa huo. "Hatungelifanya zoezi hilo mchana kweupe na mbele ya mashahidi", afisa mwengine serikalini amesema.

Familia za watu waliouawa zinaomba uchunguzi huru ufanyike haraka

Shahidi mwingine, amesema aliona makaburi matatu mbali kabisa na makaburi yanayotambuliwa rasmi, katika msitu wa Rukoko. Nyasi zimeanza kuota sehemu hiyo. Shahidi huu anaelezea kile alichokiona Desemba 11 na ana imani kuwa ni makaburi ya halaiki.

"Desemba 11, saa 11:30 niliaona lori la polisi ambalo lilikuja na maiti na kisha Walipofika eneo hilo, walichimbwa makaburi matano. Kila kaburi moja, waliweka maiti tatu".

Polisi yakanusha

Msemaji wa polisi Pierre Nkurikiye amekanusha kuwa polisi haikuzika maiti yoyote. "Ilikuwa ni kazi ya utawala", Pierre Nkurikiye amesema. "Wawambiye sehemu ambapo kuna makaburi ya halaiki na twenda pamoja kuangalia. Je, kuna weza kuwa makaburi ya halaiki ambayo hayajulikani na polisi? Haiwezekani", Pierre Nkurikiye ameongeza.

Hali ya usalama imeendelea kudorora katika maeneo mengi nchini Burundi hasa, mjini Bujumbura, Milio ya risasi na milipuko ya guruneti vimesikika usiku wa Jumanne kuamkia leo Jumatano kuamkia katika wilaya ya Nyakabiga na Bwiza jijini kati Bujumbura. Inasemekana kuwa kituo cha polisi kimeshambuliwa na watu wenye silaha wilayani Nyakabiga.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.