Pata taarifa kuu
BURUNDI-CNARED-MAZUNGUMZO

Burundi: Mazungumzo kati ya serikali na upinzani kuanza Uganda

Wawakilishi wa serikali, upinzani na vyama vya kiraia nchini Burundi wameelekea Jumapili hii nchini Uganda ambapo kunaanzishwa leo Jumatatu Desemba 28 mazungumzo kuhusu mgogoro unaendelea kushuhudiwa nchini humo, wanadiplomasia wametangaza.

Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza na Rais wa Uganda Yoweri Museveni mjini Bujumbura, wakati wa awamu ya kwanza ya mazungumzo yaliofeli, Julai 14, 2015.
Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza na Rais wa Uganda Yoweri Museveni mjini Bujumbura, wakati wa awamu ya kwanza ya mazungumzo yaliofeli, Julai 14, 2015. © RFI/Sonia Rolley
Matangazo ya kibiashara

"Mazungumzo juu ya mustakabali wa Burundi yatazinduliwa rasmi Jumatatu hii katika mji wa Entebbe", ambapo kunapatikana Ikulu ya rais, karibu na mji mkuu wa Kampala, Waziri wa Ulinzi wa Uganda Krispo Kiyonga, ameliambia shirika la habari la Ufaransa laAFP.

"Pande zote zitakuwepo, ikiwa ni pamoja na serikali ya Burundi", Waziri huyo amesema, akithibitisha kuwa mazungumzo hayo yatafanyika chini ya uangalizi wa rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni, mpatanishi aliyeteuliwa na Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Burundi imekumbwa na mgogoro mkubwa wa kisiasa tangu rais Pierre Nkurunziza kuchukua uamzi wa kugombea katika uchaguzi wa urais mwishoni mwa mwezi Aprili, ambaye alichaguliwa mwezi Julai - kwa mhula wa tatu, ambapo upinzani, vyama vya kiraia na baadhi ya vigogo na wafuasi wengine katika chama chake cha CNDD-FDD wanadai ni kinyume na Katiba ya nchi hiyo na Mkataba wa amani na maridhiano wa Arusha uliomaliza vita vya wenyewe kwa mwaka 2006.

Muungano wa wanasiasa na wanaharakati wa vyama vya kiraia waliokimbilia nje ya nchi, Cnared, unaopinga muhula wa tatu wa Pierre Nkurunziza, pia umealikwa kushiriki katika mazungumzo hayo.

Mpaka sasa, serikali ya Burundi ilikua imekataa kushiriki katika mamazungumzo na Cnared, ikiita "kuundi la kigaidi" na kuituhumu kuwa ilishiriki katika mapinduzi yaliyoshindwa mwezi Mei pamoja na mashambulizi yanayoendelea dhidi ya vikosi vya usalama.

Mwezi Julai, jaribio la awali la majadiliano kati ya serikali na upinzani lilishindwa, baada ya wawakilishi wa chama na serikali kujiondoa siku mbili kabla ya uchaguzi wa rais ambao ulipelekea Pierre Nkurunziza kuchaguliwa tena.

Mambo makubwa yanatazamiwa kuanza hivi karibuni, wiki ijayo labda, kwa mujibu wa baadhi ya vyanzo vya kidiplomasia. Na wakati huu, wahusika wakuu mbalimbali wa mgogoro wa Burundi watakutana katika mji wa Arusha, nchini Tanzania. Ni katika mji huu ambapo kulisaini mwaka 2000 mkataba wa amani na maridhiano uliomaliza vita vya wenyewe kwa nchini Burundi, vita viliodumu zaidi ya mwongo mmoja.

Umoja wa Afrika (AU) ulitangaza siku nane ziliyopita kwamba itatuma ujumbe wake wa askari 5,000 nchini Burundi kujaribu kuzuia ghasia, na kuitishia serikali ya Bujumbura kwamba itatuma askari hao hata bila idhni yake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.