Pata taarifa kuu
BURKINA FASO-USALAMA

Burkina: kikosi kipya cha usalama wa rais

Kikosi kipya cha usalama wa rais kimeundwa nchini Burkina Faso baada ya kuvunjwa kwa kikosi cha zamani cha usalama wa rais kufuatia mapinduzi ya Septemba 17.

Askari wa kikosi cha zamani cha usalama wa rais, kilivunjwa baada ya jaribio la mapinduzi ya Septemba 17 kutibuliwa. Hapa ilikua Septemba 20, 2015.
Askari wa kikosi cha zamani cha usalama wa rais, kilivunjwa baada ya jaribio la mapinduzi ya Septemba 17 kutibuliwa. Hapa ilikua Septemba 20, 2015. © AFP/SIA KAMBOU
Matangazo ya kibiashara

Kikosi kipya cha usalama wa taasisi za uongozi wa nchi kilichukua madaraka wiki iliyopita. Kikosi hiki kwa sasa kinatoa ulinzi wa rais mpya wa Burkina Faso.

Kikosi cha usalama wa taasisi za uongozi wa nchi kwa sasa kinatoa usalama ulinzi wa rais wa Burkina Faso na baadhi viongozi wa taasisi mbalimbali za uongozi wa nchi. Kikosi hiki kipya kinaundwa na askari polisi na wanajeshi, na kinaoongozwa na Kanali Boukari Baguian, ambaye awali alikuwa kiongozi wa Chuo cha kijeshi cha Kadiogo, shule ya sekondari inayomilikiwa na Wizara ya Ulinzi.

Kikosi hiki kinaundwa kwa sasa na askari polisi na wanajeshi 400, lakini idadi hii itaongezwa hadi kufikia elfu.

Kwa mujibu wa chanzo cha usalama, kikosi hiki kitakua na majukumu maalum. Baadhi ya wanaounda kikosi hiki watakuwa na jukumu la usalama wa Rais, wengine watahudumuIdara za upelelezi na ujasusi au kwa kutoa ulinzi wa kutosha.

Naba Koom 2, kambi ya kikosi kipya cha usalama wa rais

Ili kudumisha mshikamano wa kikosi cha usalama wa rais, kumepangwa mfululizo wa mafunzo maalum. Kikosi hiki kipya cha usalama wa rais kinapiga kambi katika kambi ya Naba Koom 2 kambi, kambi ya kikosi cha zamani cha usalama wa rais kabla ya kuvunjwa.

Tangu kuvunjwa kwa kikosi cha zamani cha usalama wa rais Blaise Compaoré baada baada ya mapinduzi ya Septemba 17, Polisi ndio ilikua ikitoa ulinzi wa rais wa mpito, Michel Kafando.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.